Iran haina tatizo katika kuzalisha silaha za kistratijia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62895-iran_haina_tatizo_katika_kuzalisha_silaha_za_kistratijia
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Iran haina tatizo katika uzalishaji wa silaha za kistratijia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 18, 2020 21:58 UTC
  • Iran haina tatizo katika kuzalisha silaha za kistratijia

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Iran haina tatizo katika uzalishaji wa silaha za kistratijia.

Brigedia Jenerali Amir Hatami aliyasema hayo Jumanne ya jana alipokutana na wanachama wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, ambao walitembelea maonyesho ya mafanikio ya Wizara ya Ulinzi katika kuunda silaha na zana za kivita. Ameongeza kuwa, Wizara ya Ulinzi itaendeleza sera zake za kuimarisha usalama wa taifa na kudumisha uwezo wa kumzuia adui kuihujumu nchini.

Brigedia Jenerali Amir Hatami ameashiria uwezo mkubwa wa Wizara ya Ulinzi katika kukidhi mahitaji ya kiulinzi ya nchi na kusema: "Katika mwaka huu ambao nara na kauli mbiu yake ni kuongeza uzalishaji wa kiviwanda nchini, Wizara ya Ulinzi iko tayari kusaidia sekta ya uchumi na isiyo ya kijeshi."

Mkuu wa Tume ya Sera za Kigeni na Usalama wa Taifa katika Bunge la Iran akizungumza katika kikao hicho, amesema katika uga wa intaneti, vita vya kielektroniki, makombora, vita vya nchi kavu, baharini na angani, kuna hatua kubwa ambazo zimechukuliwa kwa lengo la kuiwezesha Iran kumzuia adui. Amesema vikwazo vya kimataifa vimeifanya Iran iweze kujitegemea katika sekta ya ulinzi.