-
Iran: Iwapo Israel itapora ardhi zaidi za Wapalestina itapata jibu kali la wapigania ukombozi wa Palestina
Jun 26, 2020 11:43Mshauri wa Spika wa Bunge la Iran katika masuala ya kimataifa ameuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu mpango wake wa kupora ardhi zaidi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Watu zaidi ya 177,000 walioambukizwa COVID-19 nchini Iran wapona
Jun 26, 2020 11:35Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran ametangaza kuwa, hadi hivi sasa waathirika 177,000 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona nchini Iran wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Iran: Aziomio lililopendekezwa na Marekani ni haribifu kwa Baraza la Usalama
Jun 26, 2020 11:25Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema rasimu ya azimio ambalo limependekezwa na Marekani kwa ajili ya kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran ni kinyume cha azimio 2231 na ni kosa kubwa ambalo litakuwa haribifu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Mousavi: Wairani ni wahanga wa magaidi wanaosaidiwa na kufadhiliwa na Marekani
Jun 26, 2020 03:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amejibu tuhuma na madai yasio na msingi yaliyotolewa na Marekani dhidi ya Iran akisema utawala wa Marekani ambao ndio mfadhili mkuu wa ugaidi wa kiserikali duniani hauna hadhi ya kutoa madai ya kupambana na ugaidi au kutoa hukumu na maamuzi katika uwanja huu.
-
Njama za Marekani za kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran kupitia Baraza la Usalama la UN
Jun 25, 2020 22:02Marekani imeanzisha kampeni kubwa za kimataifa za kulizuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lisitekeleze azimio lake nambari 2231 linalotoa amri ya kuiondolea Iran vikwazo vya silaha ifikapo tarehe 18 Oktoba mwaka huu wa 2020. Marekani inaendesha njama hizo kama sehemu ya kukabiliana na uwezo mkubwa wa kiulinzi na kijeshi wa Iran unaozidi kukua na kuwa imara siku baada ya siku.
-
Marekani yaendeleza uadui wake kwa kuiwekea vikwazo vyengine vipya Iran
Jun 25, 2020 21:59Wizara ya Fedha ya Marekani imeendeleza mwenendo wake wa chuki na uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuyawekea vikwazo mashirka manane yenye uhusiano na Iran.
-
Zaidi ya watu laki moja na 75,000 wameshapata afueni baada ya kuugua COVID-19 nchini Iran
Jun 25, 2020 07:16Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran amesema kuwa, hadi hivi sasa zaidi ya watu laki moja na 75 elfu wameshapata afueni baada ya kuugua ugonjwa wa COVID-19 hapa nchini na wameruhusiwa kurejea nyumbani.
-
Rouhani: Iran itasimama kidete zaidi dhidi ya ubeberu wa Marekani
Jun 25, 2020 03:31Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili litasimama kidete zaidi kukabiliana na sera za kibeberu za Marekani hata kuliko huko nyuma.
-
Jeshi la Anga la Iran lapokea ndege za kivita za 'Kauthar'
Jun 25, 2020 03:24Kikosi cha Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimepokea ndege tatu za kivita aina ya 'Kauthar' zilizotengenezwa na wataalamu wa humu nchini.
-
"Marekani kuikingia kifua Israel kumelishushia hadhi Baraza la Usalama"
Jun 25, 2020 03:19Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema hatua ya Marekani ya kuendelea kuukingia kifua na kuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel imelifanya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lipoteze hadhi yake na likose maana.