Marekani yaendeleza uadui wake kwa kuiwekea vikwazo vyengine vipya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61820-marekani_yaendeleza_uadui_wake_kwa_kuiwekea_vikwazo_vyengine_vipya_iran
Wizara ya Fedha ya Marekani imeendeleza mwenendo wake wa chuki na uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuyawekea vikwazo mashirka manane yenye uhusiano na Iran.
(last modified 2026-08-23T05:27:14+00:00 )
Jun 25, 2020 21:59 UTC
  • Marekani yaendeleza uadui wake kwa kuiwekea vikwazo vyengine vipya Iran

Wizara ya Fedha ya Marekani imeendeleza mwenendo wake wa chuki na uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuyawekea vikwazo mashirka manane yenye uhusiano na Iran.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya fedha ya Marekani imeeleza kwamba, mashirika hayo manane yana uhusiano na sekta za feleji na chuma za Iran.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa kupitia tovuti ya wizara ya fedha ya Marekani, Washington imechukua hatua ya kuyawekea vikwazo mashirika matatu ya Kiirani, mashirika matatu yenye makao yao Imarati, shirika moja lililoko Hong Kong na jengine lenye makao yake nchini Ujerumani.

Kabla ya hatua hiyo, wizara ya fedha ya Marekani ilikuwa imesha chukua hatua mara kadhaa za kuwawekea vikwazo shakhsia na mashirika ya Kiirani pamoja ya kigeni kwa visingizio mbali mbali.

Baada ya Marekani kujitoa kinyume cha sheria katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mnamo Mei 8, 2018, serikali ya Washington ilianzisha kampeni za kila upande kwa lengo la kuiweka kwenye mashinikizo na mbinyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hatua hiyo ya serikali ya Trump imelaaniwa na kukosolewa vikali ndani ya Marekani kwenyewe na katika uga wa kimataifa.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo ni moja ya mihimili mikuu ya kambi ya muqawama, ndiyo yenye kutoa mchango mkuu katika kukabiliana na njama na hatua za kiuadui za mhimili wa pande tatu za Marekani, Uzayuni na Aal Saud katika eneo la Asia Magharibi.../