-
Iran: Wanachama wa UN hawana wajibu wa kuheshimu maazimio batili dhidi ya Tehran
Sep 28, 2025 22:56Iran imesema madai yaliyotolewa na Marekani na nchi za Ulaya kuhalalisha kurejeshwa kwa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hii hayaziwajibishi nchi wanachama wa UN kuzingatia na kuheshimu hati za umoja huo zilizobatilishwa hapo awali.
-
Uganda yazilaani nchi za Magharibi kwa kulitumia Baraza la Usalama kama wenzo wa kuishinikiza Iran
Sep 28, 2025 09:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda amelaani kitendo cha nchi za Magharibi kulitumia vibaya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama wenzo wa kuishinikiza Iran, baada ya baraza hilo lenye wanachama 15 kupiga kura ya kurejesha vikwazo vya "snapback" dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Spika Qalibaf: Snapback ni batili, Iran itajibu mapigo
Sep 28, 2025 08:15Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad-Baqer Qalibaf amepinga uamilishaji wa utaratibu wa snapback wa kurejeshewa Iran vikwazo, na kuitaja hatua hiyo kuwa ni kinyume cha sheria; huku akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haina wajibu wa kuheshimu uamuzi huo ulioshinikizwa na Troika ya Ulaya.
-
Kwa nini Iran inaona utaratibu wa snapback kuwa hauna uhalali wa kisheria?
Sep 28, 2025 07:43Seyyed Abbas Araghchi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika barua yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba: Hatua ya Marekani na Troika ya Ulaya ya kurejesha maazimio ya awali ya Baraza la Usalama dhidi ya Iran haina msingi wa kisheria wala kisiasa na haikubaliwi na Tehran.
-
Kamanda wa Iran: Uchokozi wowote dhidi yetu utajibiwa haraka
Sep 28, 2025 07:32Kamanda Mkuu wa Jeshi wa Iran, Meja Jenerali Amir Hatami amesisitiza kuwa, taifa hili limejiweka sawa na tayari kutoa jibu zito na la haraka dhidi ya vitisho na vitendo vyovyote vya uhasama vya maadui dhidi yake.
-
Safavi: Marubani zaidi ya 16 wa Israel waliuawa katika vita vya siku 12
Sep 28, 2025 07:32Mshauri mkuu wa masuala ya kijeshi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, zaidi ya marubani 16 wa Israel waliangamizwa katika vita vya siku 12 vilivyotwishwa Iran na utawala wa Kizayuni.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Israel ni utawala unaodharaulika na uliotengwa pakubwa duniani
Sep 28, 2025 03:52Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameitaja Israel kama utawala unaochukiwa zaidi duniani.
-
UN yaiwekea tena Iran vikwazo vilivyokuwa vimeondolewa kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia
Sep 28, 2025 03:51Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeiwekea tena Iran vikwazo vilivyokuwa vimendolewa huko nyuma kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya 2015 katika hatua iliyochochewa na mataifa ya Ulaya bila sababu ya msingi ili kutia dosari miradi ya nyuklia ya Iran, huku baraza hilo likipuuza hatua ya nchi za Magharibi ya kuhujumu makubaliano hayo.
-
Rais wa Iran akataa matakwa ya nyuklia ya Marekani na kuyataja kuwa 'hayakubaliki'
Sep 27, 2025 23:15Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili linafadhilisha kurejeshwa kwa vikwazo kuliko kutii matakwa "yasiyokubalika" ya Marekani ya kukabidhi akiba yake yote ya urani iliyorutubishwa.
-
SEPAH: Tutaendelea kuunga mkono Muqawama hadi ukombozi wa Quds Tukufu
Sep 27, 2025 06:55Katika taarifa yake kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi Jenerali Nilforoshan na Sayyed Hassan Nasrallah, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi SEPAH limesisitiza kuwa litaendelea kuwa pamoja na imara na kambi ya Muqawama hadi Palestina na Quds Tukufu zitakapokombolewa.