-
Rais Rouhani: Ushirikiano wa kimataifa unapaswa kuchukua nafasi ya mashinikizo dhidi ya mataifa
May 04, 2020 10:56Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, ushirikiano wa pande mbili na wa kimataifa unapaswa kuchukua nafasi ya mashinikizo dhidi ya mataifa mengine kupitia ugaidi wa kiuchumi na vitisho vya kijeshi na hivyo kuandaa mazingira bora kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya kweli na vya pamoja.
-
Karibu asilimia 80 ya waliougua maradhi ya Covid-19 nchini Iran wamepata afueni
May 04, 2020 09:55Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, hadi sasa watu 79,397 waliokuwa wamekumbwa na kirusi cha corona wamepata afueni na kuruhusiwa kutoka hospitali, ikiwa ni karibu ya asilimia 80 ya watu wote waliokuwa wameambukizwa kirusi hicho.
-
Zaidi ya wagonjwa 78 elfu wa COVID-19 wamepona nchini Iran
May 04, 2020 01:31Wizara ya Afya, Matibabu na Mafunzo ya Tiba ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa waathiriwa 78 elfu na 422 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata nafuu na afya njema na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Larijani: Nchi za Magharibi zinalitazama janga la corona kibiashara
May 03, 2020 21:57Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu, Bunge la Iran, amesema katika kadhia ya ugonjwa wa corona (COVID-19), ubinadamu umeporomoka na kadhia hii inatazamwa kibiashara.
-
Rais Rouhani: Kuenea corona kumeziweka chini ya alama ya kuuliza siasa za kimataifa
May 03, 2020 07:23Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuenea kirusi cha corona kumeziweka chini ya alama ya kuuliza siasa za kimataifa na kusisitiza kuwa, leo hii walimwengu wanasema bila ya kificho kuwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran si vya kibinadamu na wanavilaani.
-
Boroujerdi: Ujerumani imeshinikizwa na Marekani idai Hizbullah ya Lebanon ni kundi la 'kigaidi'
May 03, 2020 07:07Mjumbe wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, hatua ya serikali ya Ujerumani ya kudai kuwa Hizbullah ya Lebanon ni kundi la "kigaidi" imechukuliwa kwa mashinikizo ya Marekani.
-
Shamkhani: JCPOA itakufa kikamilifu iwapo vikwazo vya silaha dhidi ya Iran vitarefushwa
May 03, 2020 03:46Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameonya kuwa, iwapo azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakiukwa kwa kuongezwa muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Tehran, basi makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yatakufa daima.
-
Iran: Marekani haina misingi ya kisheria kujifanya mshiriki wa JCPOA
May 03, 2020 03:41Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Taasisi za Kimataifa mjini Vienna amesema jitihada za Marekani za kutaka kuionesha dunia kuwa ingali mshiriki wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hazina misingi ya kisheria.
-
Zarif: Muibuaji mkubwa zaidi wa vita duniani anaiogopa Iran
May 02, 2020 22:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Marekani ni muuzaji mkubwa zaidi wa silaha duniani na pia ina bajeti ya juu zaidi ya kijeshi kati ya mataifa yote ya dunia lakini pamoja na hayo ina wasi wasi kuhusu Iran kuondolewa vikwazo vya silaha."
-
Zaidi ya wagonjwa 77 elfu wa COVID-19 wamepona nchini Iran
May 02, 2020 22:05Wizara ya Afya, Matibabu na Mafunzo ya Tiba ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa waathiriwa 77 elfu na 350 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata nafuu na afya njema na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.