-
Zarif: Muibuaji mkubwa zaidi wa vita duniani anaiogopa Iran
May 02, 2020 22:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Marekani ni muuzaji mkubwa zaidi wa silaha duniani na pia ina bajeti ya juu zaidi ya kijeshi kati ya mataifa yote ya dunia lakini pamoja na hayo ina wasi wasi kuhusu Iran kuondolewa vikwazo vya silaha."
-
Zaidi ya wagonjwa 77 elfu wa COVID-19 wamepona nchini Iran
May 02, 2020 22:05Wizara ya Afya, Matibabu na Mafunzo ya Tiba ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa waathiriwa 77 elfu na 350 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata nafuu na afya njema na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Iran: Tuko tayari kuwanufaisha wengine uzoefu tuliopata wa kukabiliana na corona
May 02, 2020 03:22Mkuu wa Komandi Kuu ya Majeshi ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuyanufaisha mataifa mengine uzoefu wake katika suala la kupambana na ugonjwa wa COVID-19.
-
Kiongozi Muadhamu atuma salamu za kuenzi Siku ya Mwalimu nchini Iran
May 01, 2020 09:16Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Mwalimu nchini Iran na kusema kuwa walimu wote, maskulini, vyuoni na katika Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) wanafanya kazi kubwa ya kulea vipaji vya watoto na mabarobaro katika njia ya matukufu ya Kiislamu na Kimapinduzi kwa shabaha ya kuunda jamii ya kidini, yenye uadilifu na yenye malengo makuu matukufu.
-
Zaidi ya wagonjwa 76 elfu wa corona wapata afueni na kutoka hospitalini nchini Iran
May 01, 2020 09:12Wizara ya Afya, Matibabu na Mafunzo ya Tiba ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa wagonjwa 76 elfu na 318 wameshapata afueni na kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kuugua ugonjwa wa COVID-19 humu nchini.
-
Kuheshimiwa dini za waliowachache nchini Iran
May 01, 2020 03:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa ripoti ambayo hutolewa kila mwaka na Marekani kwa kisingizo cha uhuru wa kuabudu ni uingiliaji wa wazi wa masuala ya ndani ya nchi nyingine kwa msingi wa habari potofu, hivyo ameilaani ripoti hiyo na kusema haikubaliki kabisa.
-
Iran: Hatua ya Ujerumani dhidi ya Hizbullah inahudumia malengo ya Israel na Marekani
May 01, 2020 02:50Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani hatua ya chuki ya serikali ya Ujerumani ya kuiita Harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi na kusema kwamba, uamuzi huo unahudumia malengo ya utawala haramu wa Israel na Marekani.
-
Jack Straw: Juhudi za Marekani za kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran hazitofanikiwa
Apr 30, 2020 20:09Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Uingereza amesema kuwa, juhudi za viongozi wa Marekani za kujaribu kuulazimisha Umoja wa Mataifa urefushe vikwazo vya silaha dhidi ya Iran ni ushari na hazitofanikiwa.
-
Makubaliano ya JCPOA; kuanzia kushindwa “mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa” hadi “ndoto za alinacha” za Mike Pompeo
Apr 30, 2020 20:09Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, juhudi za Marekani za kutaka kuongezwa muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran zinakwenda kinyume na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Rais Rouhani: Iran imefanikiwa katika makabiliano na kudhibiti Corona
Apr 30, 2020 07:23Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa Iran imefanikiwa pakubwa katika kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 ikilinganishwa na nchi nyingine za dunia.