Kiongozi Muadhamu atuma salamu za kuenzi Siku ya Mwalimu nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i60718-kiongozi_muadhamu_atuma_salamu_za_kuenzi_siku_ya_mwalimu_nchini_iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Mwalimu nchini Iran na kusema kuwa walimu wote, maskulini, vyuoni na katika Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) wanafanya kazi kubwa ya kulea vipaji vya watoto na mabarobaro katika njia ya matukufu ya Kiislamu na Kimapinduzi kwa shabaha ya kuunda jamii ya kidini, yenye uadilifu na yenye malengo makuu matukufu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 01, 2020 09:16 UTC
  • Kiongozi Muadhamu atuma salamu za kuenzi Siku ya Mwalimu nchini Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Mwalimu nchini Iran na kusema kuwa walimu wote, maskulini, vyuoni na katika Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) wanafanya kazi kubwa ya kulea vipaji vya watoto na mabarobaro katika njia ya matukufu ya Kiislamu na Kimapinduzi kwa shabaha ya kuunda jamii ya kidini, yenye uadilifu na yenye malengo makuu matukufu.

Leo Ijumaa tarehe Mosi Mei inasadifiana na siku aliyouawa shahidi mwanafalsafa, mwanachuoni wa kidini na mhadhiri wa Chuo Kikuu, Shahid Murtadha Mutahhari na siku hii katika kalenda ya Iran inajulikana kuwa ni Siku ya Mwalimu humu nchini.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika ujumbe wake huo kwamba mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu umeanzishwa kwa lengo la kuunda jamii ya kidini, ya kiuadilifu na yenye malengo makuu matukufu na kwamba watoto wadogo, mabarobaro na vijana wa Iran ya Kiislamu wanafundishwa kwamba watumie vipaji na vipawa vyao katika kutumikia matukufu makuu ya kitaifa yaani matukufu ya Kiislamu na ya Kimapinduzi.

mutahhari

Siku ya Mwalimu ni muhimu sana nchini Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, mafundisho hayo muhimu sana ndiyo kazi kubwa na ya kijihadi inayofanywa na walimu.

Ayatullah Khamenei aidha amesema, Uislamu unatuhimiza kutafuta elimu yenye manufaa. Kwa upande mmoja elimu hiyo yenye manufaa kwa upande mmoja inamuandalia kijana wa Kiirani vifaa anavyohitajia kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa nchi na kwa upande mwingine inampa kijana huyo utambulisho wake, heshima na itibari ya kiroho na kimaanawi pamoja na nguvu za kujiamini.

Vile vile amesema kuwa, Alhamdulillah vijana wa Iran wana vigezo bora kabisa ambavyo ni nadra kuonekana katika uliwemwengu wa leo unaopenda mambo ya kidunia na kumalizia kwa kusema kwamba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwaendee mashahidi na shukrani zetu ziende kwa walimu na pongezi zetu ziende kwa vijana wa taifa la Iran wenye mustakbali bora mbele yao.