-
Zarif: Jukumu la kisheria la serikali ya Iraq ni kuzilinda balozi ndogo za Iran
Dec 05, 2019 03:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuhusiana na shambulio la karibuni dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Najaf kuwa: Jukumu la kisheria la serikali ya Iraq ni kuzilinda balozi ndogo za Iran.
-
Kamanda Fadavi: Akthari ya wafanya ghasia, walitiwa mbaroni wakijaribu kutoroka Iran
Dec 04, 2019 21:52Kaimu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Ali Fadavi amesema kuwa akthari ya wafanya ghasia za hivi kariuni walitiwa mbaroni wakati wakijaribu kutoroka Iran.
-
Tehran yatoa onyo kali kwa maadui: Msivuke mistari myekundu ya Iran
Dec 04, 2019 08:36Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ametoa onyo kali kwa maadui akiwaambia wasivuke mistari myekundu ya Iran.
-
Rouhani: Mazungumzo na kundi la 5+1 yanawezekana iwapo vikwazo vya kidhalimu dhidi ya Iran vitaondolewa
Dec 04, 2019 04:23Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na viongozi wa kundi la 5+1 iwapo Marekani italiondolea taifa hili vikwazo vyake vya kidhalimu.
-
Rouhani: Marekani ni nchi inayotenda jinai na ya kigaidi
Dec 03, 2019 08:52Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vikwazo vikali vya Marekani dhidi ya taifa la Iran na kueleza kuwa Marekani ni nchi inayotenda jinai na ya kigaidi.
-
Mkurugenzi Mkuu mpya wa wakala wa IAEA na mustakabali wa JCPOA
Dec 03, 2019 08:38Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ukiwa asasi ya usimamizi ya Umoja wa Mataifa kwa taasisi na shughuli za nyuklia za nchi wanachama, una nafasi muhimu mno katika kudhamini shughuli za nyuklia za wanachama wake na vilevile kueneza matumizi ya nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani.
-
Rouhani: Nchi za Asia Magharibi zinapasa kuwajibika ipasavyo katika kudhamini usalama wa eneo
Dec 03, 2019 08:34Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa nchi za eneo la Asia Magharibi zinapasa kushiriki katika kudhamini usalama wa eneo na kuwajibika ipasavyo katika uwanja huo. Amesema Iran imewasilisha Mpango wa Amani ya Hormoz kwa mtazamo huo.
-
Mkuu mpya wa IAEA ataka uhusiano chanya na Iran
Dec 03, 2019 04:21Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema ana matarajio makubwa kwamba taasisi hiyo itakuwa na uhusiano chanya na amilifu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kudhamini usalama kwa pamoja katika eneo, ajenda ya mashauriano kati ya Zarif na Bin Alawi mjini Tehran
Dec 03, 2019 03:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Yusuf bin Alawi bin Abdullah amekutana na kufanya mazungumzo na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran hapa mjini Tehran. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jana, Zarif na Bin Alawi walibadilishana mawazo kuhusu masuala ya kieneo na kimataifa. Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miezi tisa iliyopita kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman kufanya safari hapa mjini Tehran.
-
Zarif azilaumu nchi za Ulaya kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kibinadamu
Dec 02, 2019 23:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezilaumu nchi za Ulaya kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kibinadamu na kuongeza kuwa, ni jukumu la nchi za Ulaya kutekeleza wajibu wa kuhusu watoto wadogo wa Iran wanaokwama kwenye matibabu kutokana na ugaidi wa kiuchumi unaofanywa na Marekani dhidi ya wananchi wa taifa hili.