Rouhani: Marekani ni nchi inayotenda jinai na ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i57655-rouhani_marekani_ni_nchi_inayotenda_jinai_na_ya_kigaidi
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vikwazo vikali vya Marekani dhidi ya taifa la Iran na kueleza kuwa Marekani ni nchi inayotenda jinai na ya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 03, 2019 08:52 UTC
  • Rouhani: Marekani ni nchi inayotenda jinai na ya kigaidi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vikwazo vikali vya Marekani dhidi ya taifa la Iran na kueleza kuwa Marekani ni nchi inayotenda jinai na ya kigaidi.

Akizungumza leo hapa Tehran mbele ya hadhara ya watu wenye ulemavu sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, Rais Hassan Rouhani ameongeza kuwa Marekani imeweka vikwazo hivyo ambavyo havijawahi kushuhudiwa kama inavyokiri nchi hiyo hivyo ni vikwazo vikali zaidi vya kiuchumi dhidi ya Iran lengo lake likiwa ni kulipigisha magoti taifa hili. 

Watu wenye ulemavu wakisikiliza hotuba ya Rais Rouhani mjini Tehran

Rais Rouhani amesema kuwa wananchi wa Iran wamelinda heshima yao, wamevuka hali ngumu na kuibuka na ushindi kutokana na kuwa kwao imara na kuvumilia machungu licha ya mashinikizo yote hayo magumu ya kiuchumi na vikwazo visivyo vya kiadilifu dhidi ya nchi hii.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa muqawama wa  wananchi wa Iran umeipelekea Marekani hii leo kutaka kufanya mazungumzo na nchi hii huku ikituma jumbe binafsi katika uwanja huo. Amesema jumbe na maombi hayo yanayotumwa na Marekani kwa ajili ya mazungumzo na Iran ni kinyume na nara zinazotamkwa hadharani; na nchi za Ulaya ambazo zimekuwa kiunganishi pia zinafahamu vyema jambo hilo. Umoja wa Mataifa umeitangaza tarehe Tatu Disemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Maadhimisho ya Watu wenye Ulemavu.