-
Mkuu mpya wa IAEA ataka uhusiano chanya na Iran
Dec 03, 2019 04:21Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema ana matarajio makubwa kwamba taasisi hiyo itakuwa na uhusiano chanya na amilifu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kudhamini usalama kwa pamoja katika eneo, ajenda ya mashauriano kati ya Zarif na Bin Alawi mjini Tehran
Dec 03, 2019 03:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Yusuf bin Alawi bin Abdullah amekutana na kufanya mazungumzo na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran hapa mjini Tehran. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jana, Zarif na Bin Alawi walibadilishana mawazo kuhusu masuala ya kieneo na kimataifa. Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miezi tisa iliyopita kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman kufanya safari hapa mjini Tehran.
-
Zarif azilaumu nchi za Ulaya kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kibinadamu
Dec 02, 2019 23:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezilaumu nchi za Ulaya kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kibinadamu na kuongeza kuwa, ni jukumu la nchi za Ulaya kutekeleza wajibu wa kuhusu watoto wadogo wa Iran wanaokwama kwenye matibabu kutokana na ugaidi wa kiuchumi unaofanywa na Marekani dhidi ya wananchi wa taifa hili.
-
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Oman wafanya mazungumzo mjini Tehran
Dec 02, 2019 09:04Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Oman ambaye yupo safarini hapa Tehran, leo amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran.
-
Kuanza uandikishaji wa wagombea uchaguzi wa Bunge la 11 la Iran
Dec 02, 2019 08:02Uandikishaji watu wanaotaka kugombea ubunge katika uchaguzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, yaani Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ulianza rasmi jana Jumapili na utaendelea hadi tarehe 7 ya mwezi huu wa Desemba.
-
Watu 789 wajiandikisha kuwania ubunge Iran katika siku ya kwanza ya usajili
Dec 02, 2019 03:53Msemaji wa Makao Makuu ya Uchaguzi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran amesema: "Katika siku ya kwanza ya kujiandikisha wagombea katika awamu ya 11 Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, watu 789 wamejisajili.
-
Zoezi la kujiandikisha wanaotaka kugombea ubunge Iran laanza
Dec 02, 2019 01:10Zoezi la uandikishaji wagombea wa uchaguzi wa awamu ya 11 Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, limeanza rasmi Jumapili.
-
Larijani: Watawala wa Marekani lazima wasitishe sera ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran
Dec 01, 2019 09:15Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, 'Bunge la Iran' amesema sera ya Marekani ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Iran ni ghalati na ni lazima watawala wa Marekani wasitishe sera hiyo.
-
Iran na China zafanya mazungumzo kuhusu JCPOA
Dec 01, 2019 03:51Iran na China zimekutana katika kikao cha mashauriano kuhusu namna ya kulinda vipengee vya mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Nyambizi za Jeshi la Wanamaji la Iran zasheheniwa makombora ya cruise ya Jask-2 yaliyotengezwa nchini
Nov 30, 2019 23:36Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, makombora ya cruise aina ya Jask-2 yaliyotengezwa nchini, sasa yanazalishwa kwa wingi na kuongeza kuwa, nyambizi zote za jeshi zitasheheniwa makombora hayo.