-
Tehran: Nchi zilizozaa ugaidi zisiibebeshe Iran matatizo yao
Nov 24, 2019 08:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu matamshi ya kipuuzi na yasiyo na msingi yaliyotolewa na baadhi ya washiriki wa kikao kilichopewa jina la "Mazungumzo ya Manama" huko Bahran na kusisitiza kuwa tuhuma zilizotolewa na watu hao dhidi ya Iran hazina msingi.
-
Mamluki wa makundi ya kigaidi ya Daesh na Pijak watiwa mbaroni magharibi mwa Iran
Nov 24, 2019 04:30Gavana wa mkoa wa Kermanshah magharibi mwa Iran ametangaza habari ya kutiwa mbaroni mamluki wa makundi ya kigaidi ya Daesh na Pijak.
-
Wananchi wa Iran waendeleza maandamano ya kulaani ghasia na fujo
Nov 24, 2019 01:02Wananchi wa Iran, sawa na siku za hivi karibuni, wameendeleza maandamano katika miji mbali mbali nchini kuwalaani waibua fujo na ghasia.
-
Hatua ya Marekani ya kumuwekea vikwazo Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Iran
Nov 23, 2019 09:00Katika kipindi cha utawala wa Rais Donald Trump, Marekani imeiwekea Iran vikwazo vikali ikiwa ni katika kutekeleza siasa zake za mashinikizo ya juu zaidi. Wakati huo huo ghasia zilizotokea hivi karibuni nchini Iran zimetumiwa na serikali ya Washington kuwawekea vikwazo vipya viongozi wa ngazi ya juu wa Iran ikiwa ni katika kuunga mkono ukosefu huo wa amani na wasababishaji wa ghasia hizo.
-
Jahangiri: Iran itatoa jibu kali kwa nchi zinazoingilia mambo yake ya ndani
Nov 23, 2019 08:20Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadahrisha kuwa: "Iwpao itathibiti kuwa nchi za eneo zimehusika katika ghasia na machafuko ya hivi karibnu nchini Iran, basi bila shaka zitapokea jibu kali."
-
Waziri wa TEHAMA Iran: Vikwazo vya Marekani haviwezi kuzuia maendeleo Iran
Nov 23, 2019 08:16Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Iran mapema Jumamosi ametoa kauli baada ya jina lake kuwekwa katika orodha ya vikwazo vya Marekani na kusisitiza kuwa, Washington haiwezi kuzuia maendeleo na ustawi nchini Iran.
-
Mashtaka ya Tehran dhidi ya kanali za Uingereza zinazochochea fujo nchini Iran
Nov 23, 2019 04:25Hamid Baeidinejad, Balozi wa Iran mjini London ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba, Tehran imezishitaki kanali za maadui wa taifa la Iran za Uingereza ambazo zinatangaza kwa lugha ya Kifarsi kama vile BBC ya Kifarsi, kanali ya Iran International inayofadhiliwa na Saudi Arabia na ile ya Manoto, kutokana na kupotosha kwa makusudi matukio ya hivi karibuni humu nchini.
-
Iran yazifungulia mashtaka kanali za Uingereza kwa kuchochea ghasia nchini
Nov 22, 2019 23:12Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia ubalozi wake mjini London, Uingereza imewasilisha mashtaka kwa Idara ya Mawasiliano ya Uingereza OFCOM dhidi ya kanali za upinzani zinazotangaza kwa lugha ya Kifarsi za nchi hiyo, kutokana na kupotosha kwa makusudi matukio ya hivi karibuni nchini hapa.
-
Meja Jenerali Rashid: Ili kulinda roho za askari wake, Marekani inapasa kuchunga mienendo yake
Nov 22, 2019 23:10Kamanda wa kituo cha Khatamul-Anbiya (saw) cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ili kulinda roho za askari wake, Marekani inapasa kujiepusha na mienendo ghalati katika eneo la Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormoz.
-
Wairani waandamana nchi nzima kulaani ghasia za hivi karibuni
Nov 22, 2019 10:28Raia wa Iran wamefanya maandamano makubwa baada ya swala ya Ijumaa kwa kupiga nara za 'Mauti kwa Marekani', 'Mauti kwa Israel' na 'Mauti kwa wafanya vurugu' ambapo pia sambamba na kutangaza kujitenga mbali na wafanya ghasia na kuchukia vitendo viovu vya kuibua machafuko nchini, wametangaza kuunga mkono usalama na amani nchini.