-
Iran itajibu chokochoko katika maji ya kimataifa baada ya meli yake kushambuliwa
Oct 12, 2019 08:32Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametoa tamko kufuatia kulengwa meli ya mafuta ya Iran katika Bahari ya Sham na kusisitiza kuwa: "Uharamia na chokochoko katika maji ya kimataifa hazitabakia bila jibu."
-
Salami: Adui hana nguvu yoyote mbele ya taifa la Iran
Oct 12, 2019 04:33Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kuwa maadui hawana dira wala nguvu yoyote mkabala wa taifa imara la Iran.
-
Mpango wa amani wa Zarif kwa ajili ya Ghuba ya Uajemi, mbinu na mambo ya lazima
Oct 12, 2019 03:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, iwapo nchi za Ghuba ya Uajemi zitawekeana mkataba wa kutoshambuliana wala kuingilia masuala ya ndani ya upande mwingine, mkataba huo unaweza kuleta amani, usalama, utulivu na ustawi wa kudumu kwa nchi zote za eneo hilo.
-
Iran yakaribisha mazungumzo na Saudi Arabia
Oct 11, 2019 23:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekaribisha juhudi za upatanishi za kuandaa mazungumzo baina ya Tehran na Saudi Arabia zikiwemo zile zinazofanywa na Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan, ambaye leo Jumamosi anatarajiwa kuwasili hapa Tehran kwa ajili ya kuonana na viongozi wa ngazi za juu wa Iran.
-
Iran: Dhima ya kushambuliwa meli yetu ya mafuta iko kwa wafanya chokochoko
Oct 11, 2019 07:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza hisia zake baada ya kushambuliwa meli ya mafuta ya Iran katika Bahari Nyekundu na kusema kuwa, dhima yote ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na uchafuzi mkubwa wa mazingira uliosababishwa na kushambuliwa meli hiyo iko juu ya wanaofanya chokochoko kwenye eneo hili.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Wahusika wakuu wa machafuko ya karibuni Iraq ni Marekani, Uingereza na Israel
Oct 11, 2019 07:22Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, wahusika wakuu wa machafuko ya hivi karibuni nchini Iraq ni pembe tatu za shari duniani ambazo ni Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kiongozi Muadhamu katika mkutano na vijana wenye vipaji vya kisayansi asisitiza kuhusu ustawi wa kasi kisayansi
Oct 11, 2019 04:42Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumatano alikutana na wasomi elfu mbili vijana wenye vipaji vya kisayansi na kielimu wa Iran na kutilia mkazo udharura wa kudumishwa maendeleo ya kielimu ya Iran katika harakati inayokwenda kwa kasi ya kisayansi duniani.
-
Iran: Tunakaribisha ushirikiano wa kuheshimiana baina yetu na Umoja wa Ulaya
Oct 10, 2019 23:13Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inapokea vizuri ushirikiano wenye nia njema na wa kuheshimiana baina yake na Umoja wa Ulaya.
-
Mazoezi ya jeshi la Iran, maonyesho ya nguvu za Jamhuri ya Kiislamu yenye ujumbe wa amani
Oct 10, 2019 05:22Mazoezi ya Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu yamefanyika katika eneo la kaskazini magharibi mwa Iran yakiwa na lengo la kuonesha utayarifu wa jeshi hilo, uwezo na nguvu zake sambamba na kutoa ujumbe wa amani.
-
Spika wa Bunge la Iran aghairisha safari yake ya Uturuki baada ya nchi hiyo kuivamia kijeshi Syria
Oct 10, 2019 04:21Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ameghairisha safari aliyokuwa amepanga kufanya nchini Uturuki kufuatia hatua ya nchi hiyo ya kuivamia kijeshi ardhi ya Syria.