Iran itajibu chokochoko katika maji ya kimataifa baada ya meli yake kushambuliwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56576-iran_itajibu_chokochoko_katika_maji_ya_kimataifa_baada_ya_meli_yake_kushambuliwa
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametoa tamko kufuatia kulengwa meli ya mafuta ya Iran katika Bahari ya Sham na kusisitiza kuwa: "Uharamia na chokochoko katika maji ya kimataifa hazitabakia bila jibu."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 12, 2019 08:32 UTC
  • Iran itajibu chokochoko katika maji ya kimataifa baada ya meli yake kushambuliwa

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametoa tamko kufuatia kulengwa meli ya mafuta ya Iran katika Bahari ya Sham na kusisitiza kuwa: "Uharamia na chokochoko katika maji ya kimataifa hazitabakia bila jibu."

Meli ya Mafuta ya Iran inayojulikana kama SABITY, Ijumaa asubuhi, ikiwa inapita katika njia maalumu ya meli za mafuta mashariki mwa Bahari ya Sham, ililengwa mara mbili kwa makombora katika kipindi cha masaa mawili.

Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran leo amesema kitendo hicho kimelenga kuvuruga usalama wa usafiri wa meli za kibiashara na kuongeza kuwa: "Uchunguzi wa klipu za video na ushahidi wa kiintelijensia uliokusanywa, umebaini wahusika wakuu wa chokochoko hiyo hatari."

Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran

Shamkhani ameongeza kuwa: "Kamati maalumu imebuniwa kuchunguza hujuma dhidi ya meli ya mafuta ya SABITY  ambayo imelengwa kwa makombora mawili ikiwa inapita karibu na pwani ya Saudia na ripoti kuhusu tukio hilo itakabidhwa wahusika ili waweze kuchukua uamuzi."

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran aidha ameashiria hatua haribifu za miezi ya hivi karibuni dhidi ya meli za mafuta za Iran za Happiness na HELM katika Bahari ya Sham na kusema: "Kuvuruga usalama wa maji ya kimataifa kutakuwa na taathira zenye kutia wasiwasi katika uchumi wa dunia."

Shamkhani amesisitiza kuwa waliotekeleza na kupanga chokochoko hizo watajuta.