-
Simulizi ya daktari Mmarekani aliyerejea kutoka Gaza; mauaji makubwa ya kimbari yanajiri katika eneo hilo
Aug 10, 2025 05:23Mark Browner, daktari wa Marekani aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza, amesema katika taarifa yake kwamba mauaji makubwa ya kimbari yanatokea katika eneo hilo na kwamba watu wengi wameaga dunia kwa njaa hivi karibuni katika eneo hilo.
-
Albanese: Tutakomesha mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina
Aug 10, 2025 05:22Francesca Albanese Ripota wa Umoja wa Mataifa amesisitiza dhamira yake na ya watu wengine wenye dhamira kama hiyo juu ya kusitisha mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa huko Gaza na utawala wa Israel. Albanese ameulaani utawala wa Israel na kuutaja kuwa unawafanyia udikteta wananchi wa Palestina.
-
Witkoff na Waziri Mkuu wa Qatar wajadili masuala wanayohitilafiana Hamas na Israel
Aug 10, 2025 05:21Gazeti la Israel Hayom limeandika kuwa: Mjumbe Maalumu wa Marekani Steve Witkoff na Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mohammed bin Abdulrahman Al Thani wamekutana na kujadili huko Uhispania njia za kutatua hitilafu zilizopo kati ya harakati ya Hamas na utawala wa Israel.
-
Kamishna wa EU atahadharisha kuhusu mpango wa Israel wa kupanua mashambulizi yake huko Gaza
Aug 10, 2025 05:20Hadja Lahbib Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya usawa, maandalizi na ufuatiliaji wa migogoro ameeleza kuwa uamuzi wa utawala wa Israel wa kupanua mashambulizi yake ya kijeshi huko Gaza utashadidisha zaidi hali ya kibinadamu katika eneo hilo na kuhatarisha maisha ya mateka waliosalia.
-
Mpango wa kuipokonya silaha Hizbullah, kosa la kimkakati kwa serikali ya Lebanon
Aug 10, 2025 04:47Waziri wa Habari wa Lebanon, Paul Morcos amesisitiza katika hotuba yake kwamba: "Baraza la mawaziri la serikali limeidhinisha kubakisha silaha mikononi mwa majeshi ya serikali tu na kutumwa jeshi kusini mwa nchi."
-
Oman yalaani uamuzi wa Israel wa kuikalia kwa mabavu Gaza
Aug 09, 2025 23:06Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman imelaani uamuzi wa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa kuukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza.
-
Mossad na Shabak zapinga mpango wa kuikalia kwa mabavu Gaza
Aug 09, 2025 11:49Wakuu wa Shirika la Ujasusi la Israel (MOSSAD) na Idara ya Ujasusi wa Ndani Shin Bet (SHABAK) zimepinga mpango wa kuukalia kwa mabavu mji wa Gaza kutokana na taathira zake mbaya.
-
OIC yaonya: Mpango wa Israel wa kuikalia kwa mabavu Gaza ni "jinai za kivita"
Aug 09, 2025 07:00Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali uamuzi wa Israel wa kukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza na kuwaondoa kwa nguvu karibu Wapalestina milioni moja kutoka Gaza City na maeneo ya kaskazini mwa kusini, na kuuita mpango huo kuwa ni "jinai dhidi ya ubinadamu."
-
UEFA yamuenzi 'Pele wa Palestina' aliyeuliwa na jeshi la Israel Ghaza wakati anangojea chakula
Aug 09, 2025 04:11Muungano wa Vyama vya Soka vya Ulaya UEFA, umemuenzi nahodha na nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Palestina Suleiman al-Obeid, ambaye aliuawa shahidi katika shambulizi la kinyama la utawala wa kizayuni wa Israel alipokuwa akisubiri msaada wa chakula huko Ghaza siku ya Jumatano.
-
Mbunge wa Hizbullah: Kukubali tupokonywe silaha ni sawa na kujinyonga
Aug 09, 2025 03:52Mbunge wa Lebanon kutoka mrengo wa kisiasa wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchi hiyo Hizbullah amelipinga vikali dai la kuitaka harakati hiyo iweke chini silaha zake kufuatia shinikizo la Marekani kwa serikali la kuitaka iipokonye silaha harakati hiyo.