Albanese: Tutakomesha mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina
Francesca Albanese Ripota wa Umoja wa Mataifa amesisitiza dhamira yake na ya watu wengine wenye dhamira kama hiyo juu ya kusitisha mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa huko Gaza na utawala wa Israel. Albanese ameulaani utawala wa Israel na kuutaja kuwa unawafanyia udikteta wananchi wa Palestina.
Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ameeleza haya katika mahojiano na televisheni ya Press ya hapa nchini.
"Tutakomesha mauaji hayo ya kimbari," ameahidi Francesca Albanese.
"Watu na taasisi mbalimbali wanajitokeza ili kuonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina na si kudhihirisha mshikamano na mimi,' ameongeza kusema Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
Amesema, haki ya Wapalestina ya kujitawala na kujiamulia mustakbali wao wa kisiasa haiko kwenye mazungumzo, licha ya jitihada kubwa zinazotekeleza na serikali ya Israel na washirika wake, hasa Marekani ili kubatilisha haki hizo kwa kuzifananisha na "ugaidi."
Amesisitiza kuwa Israel inapasa kuwekewa vikwazo kama pande yoyote inayotenda jinai.
Mwezi Machi mwaka jana, Francesca Albanese aliulipata utawala huo na hatia kwa kutekeleza vitendo visivyopungua vitatu vya mauaji ya kimbari na kuvitaja vitendo vyote hivyo kuwa mauaji na matukio yaliyoratibiwa kwa lengo la kuwaangamiza watu katika Ukanda wa Gaza.