Oman yalaani uamuzi wa Israel wa kuikalia kwa mabavu Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129354
Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman imelaani uamuzi wa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa kuukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza.
(last modified 2025-08-10T02:36:53+00:00 )
Aug 10, 2025 02:36 UTC
  • Oman yalaani uamuzi wa Israel wa kuikalia kwa mabavu Gaza

Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman imelaani uamuzi wa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa kuukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman imesisitiza katika taarifa yake kuwa inalaani vikali uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kuukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza na kuendelea kukiuka sheria za kimataifa na kutoheshimu maazimio ya Mahakama za Kimataifa na pia kukiuka haki halali za wananchi wa Palestina. 

Tarehe 7 Agosti mwaka huu, Baraza la Mawaziri la Usalama la Israel liliidhinisha pendekezo la Waziri Mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu la kuukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza. 

Uamuzi huo wa utawala ghasibu wa Israel wa kuikalia kwa mabavu Gaza  umekosolewa na kupingwa vikali na nchi, viongozi na taasisi za kimataifa na za kutetea haki za binadamu na kusisitiza kuhusu ulazima wa kusimamisha vita dhidi ya Ukanda wa Gaza na kutekelezwa mapatano ya usitishaji vita. 

Mpango wa Netanyahu pia umekabiliwa na radiamali kubwa hasi katika duru za ndani za Israel, zikiwemo duru za kijeshi na usalama.