Jumamosi, 20 Disemba, 2025
-
Leo katika historia
Leo ni Jumamosi 29 Mfunguo Tisa Jamadithani 1447 Hijria mwafaka na 20 Disemba 2025 Miladia.
Katika siku kama ya leo miaka 105 iliyopita, aliaga dunia Mullah Fat'hullah Gharawi Isfahani maarufu kama Sheikh al-Shari'ah Isfahani, alimu, mwanazuoni, mwanamapambano na fakihi mahiri wa Kiirani. Alizaliwa mwaka 1228 Hijria Shamsia katika mji wa Isfahan ulioko katikati mwa Iran na kusoma masomo ya dini katika mji huo huo. Baada yay muda alielekea katika mji wa Mash'had kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kielimu. Mulla Fa'hullah Gharawi mwaka 1257 Hijria Shamsia alikwenda katika mji wa Najaf Iraq kwa ajili ya masomo ya juu zaidi. Mwanazuoni huyu amealifu vitabu kadhaa katika nyanja mbalimbali. Wakati wa kujiri Vita vya Kwanza vya Dunia alikuuwa miongoni mwa wanazuoni wa Iraq walioendesha mapambano ya kukabiliana na Waingereza.
Siku kama ya leo miaka 90 iliyopita, Sheikh Izzuddin Qassam aliyekuwa miongoni mwa viongozi wa harakati ya mapambano ya ukombozi wa wananchi wa Palestina dhidi ya uvamizi wa Wazayuni maghasibu na ukoloni wa Uingereza, aliuawa shahidi. Baada ya kukamilisha masomo yake ya awali huko Syria, Sheikh Qassam aliendeleza masomo yake katika Chuo Kikuu cha al Azhar huko Misri. Wananchi wa Palestina walianza mapambana dhidi ya mkoloni Mwingereza mwaka 1930 chini ya uongozi wa Sheikh Izzuddin Qassam. Hata hivyo baada ya kupita miaka kadhaa Wazayuni maghasibu walishirikiana na wakoloni wa Kiingereza na kumuuwa kigaidi kiongozi huyo wa harakati ya mapambano ya Palestina. **
Miaka 74 iliyopita katika siku kama ya leo, nchi ya Oman ilipata uhuru kufuatia makubaliano yaliyosainiwa kati ya nchi hiyo na Uingereza. Oman ina historia kongwe na hadi kabla ya kudhihiri Uislamu, nchi hiyo kuna wakati iliwahi kuwa chini ya mamlaka ya Iran. Nchi hiyo iliwekwa chini ya mamlaka ya Waislamu baada ya kuaga dunia Mtume Muhammad (saw). Karibu karne moja baadaye kundi la Khawarij lilianzisha ghasia na uasi huko Oman na kuitawala nchi hiyo kwa karne kadhaa. Baadaye Oman ikakoloniwa na Ureno na Waingereza. ***

Siku kama ya leo miaka 57 iliyopita, aliaga dunia John Steinbeck mwandishi wa riwaya wa Kimarekani baada ya kuishi kwa miaka 66. Alizaliwa mwaka 1902. Katika ujana wake Steinbeck alijishughulisha na kazi mbalimbali na hatimaye akaichagua taaluma ya uandishi. Mwandishi huyo alionesha kipaji cha hali ya juu alichokuwa nacho katika uwanja wa uandishi. Machungu ya Steinbeck katika maisha yake yalimuandalia uwanja wa kubainisha masaibu na machungu ya watu wasiojiweza katika maandishi na vitabuu vyake. Miongoni mwa vitabu vyake ni Travels with Charley, East of Eden, A Russian Jornal na Burning.
Miaka 8 iliyopita katika siku kama ya leo, Ayatullah Muhyiddin Hairi Shirazi mwakilishi wa zamani wa Shiraz katika Baraza la Wanazuoni Linalomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na Kusimamia Kazi Zake aliaga dunia. Hairi Shirazi alikuwa pia Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Shiraz. Alizaliwa katika mji wa Shiraz, Iran mwaka 1315 Hijria Shamsia. Alikipitisha kipindi cha masomo ya msingi katika mji huo. Baadaye alielekea katika mji wa Qum na kuhudhuria darsa za walimu mahiri zama hizo kama Ayatullah Burujerdi, Imam Khomeinbi, Muhaqqiq Damad na Araki. Alingia katika harakati za mapambano ya kisiasa baada ya Imam Khomeini kubaidishiwa nchini Uturuki.