-
Haaretz: Israel iliua watoto 1,000 wa Kipalestina mwezi uliopita
Jul 26, 2025 08:06Gazeti la Kizayuni la "Haaretz" limekiri Jumamosi ya leo kwamba, jeshi la utawala huo liliua watoto 1,000 katika mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza mwezi uliopita pekee.
-
Ayatullah Sistani: Mataifa ya Kiarabu na Kiislamu yachukue hatua kukabiliana na njaa kali Gaza
Jul 26, 2025 04:28Kiongozi mkuu Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, ameelezea masikitiko yake makubwa kuhusu hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota katika Ukanda wa Gaza, hususan baa la njaa linalozidi kushika kasi, na kutoa wito kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za haraka kukomesha janga hili la kusikitisha.
-
Gideon Levy: Picha za njaa huko Gaza zinakumbusha mauaji ya Holocaust na kambi za mateso
Jul 25, 2025 22:58Mwandishi wa Israel, Gideon Levy amesema kuwa taswira na picha za njaa huko Gaza, ambazo zinafichwa na vyombo vya habari vya ndani vya Israel, zinakumbusha watu walionusurika katika kambi za mateso na mauaji ya Holocaust, akisisitiza kwamba kugeuza njaa kuwa silaha halali ya vita ni hatua ya kishetani zaidi ya vita vya sasa vya Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Njaa yashadidi Ukanda wa Gaza huku Israel ikiendelea kuzuia misaada
Jul 25, 2025 07:25Ofisi ya Habari ya Serikali katika Ukanda wa Gaza imezitaka nchi zote duniani kuvunja mara moja mzingiro dhidi ya Gaza, kufungua mipaka kwa njia ya kudumu, na kuingiza misaada ya dharura , hasa unga na maziwa ya watoto wachanga, kwa ajili ya watu zaidi ya milioni 2.4 walioko chini ya mzingiro mkali ambao unatekelezwa na utawala katili wa Israel.
-
Yemen yasisitiza msimamo mmoja wa Kiislamu na Kiarabu kuokoa maisha ya watu wa Gaza
Jul 24, 2025 23:13Mahdi Al-Mashat, Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ametoa wito kwa mataifa na serikali za nchi za Kiislamu na Kiarabu kuchukua msimamo na hatua madhubuti na za haraka ili kukabiliana na tishio kubwa la utawala wa kizayuni na kuokoa maisha ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.
-
Oxfam yaonya kuhusu janga la binadamu Gaza
Jul 24, 2025 23:02Shirika la kimataifa la Oxfam limeonya kuwa, maafa ya binadamu katika Ukanda wa Gaza yamefikia kiwango kisicho na kifani na njaa imeenea katika eneo zima.
-
Haaretz: Gaza imeharibiwa zaidi kuliko Hiroshima
Jul 24, 2025 08:38Katika ripoti ya kushtua iliyotegemea simulizi, picha za satelaiti na takwimu za Umoja wa Mataifa, gazeti la Israel limetangaza kuwa Gaza imeharibiwa zaidi kuliko miji ya Hiroshima na Nagasaki baada ya mashambulizi ya mabomu ya atomiki ya Marekani dhidi ya Japan.
-
HAMAS yakabidhi mapendekezo yake kuhusu makubaliano ya kusitisha vita Ghaza
Jul 24, 2025 03:22Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema katika taarifa iliyotoa mapema leo kwamba "imewasilisha majibu yake na yale ya makundi ya Wapalestina" kwa wapatanishi baada ya majuma kadhaa ya mazungumzo ya kusitisha mapigano yaliyoshindwa kuzaa matunda.
-
Zaidi ya makundi 100 ya misaada yatahadharisha njaa kali Gaza
Jul 23, 2025 23:20Zaidi ya mashirika 100 ya misaada ya kimataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yametahadharisha kuhusu njaa kali katika Ukanda wa Gaza na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti kukabiliana na hali hiyo.
-
Maafisa wa Palestina, mwanaharakati wa Ghana walaani amani ya uongo na uvamizi wa Israel
Jul 23, 2025 23:19Maafisa wa Palestina na mwanaharakati wa Ghana wamelaani unyama wa utawala wa kizayuni wa Israel huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na jinai za kila uchao zinazofanywa na utawala huo dhidi ya Wapalestina.