-
Hamas: Hatua ya Pili ya Usitishaji Mapigano Gaza ni njia pekee ya kuachiliwa mateka wa Israel
Mar 04, 2025 04:18Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, ameulaumu utawala haramu wa Israel kwa kutaka kurejesha uvamizi wake dhidi ya Gaza na kukwepa makubaliano ya usitishaji mapigano, akisisitiza kuwa njia pekee ya kuhakikisha kuachiliwa kwa mateka wa Israel ni kuanza hatua ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
-
Qatar: Kutumia chakula kama silaha ya vita ni kukiuka sheria za kimataifa
Mar 03, 2025 23:30Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imetoa taarifa na kutangaza kuwa, inapinga vikali suala la raia kufa njaa na kutumiwa chakula kama silaha ya vita katika Ukanda wa Gaza.
-
Filamu kuhusu Israel inavyowatimua Wapalestina katika ardhi yao yashinda tuzo ya Oscar
Mar 03, 2025 23:30Filamu kuhusu utawala haramu wa Israel unavyowatimua Wapalestina katika ardhi yao, imeshinda tuzo ya Oscar na wakurugenzi wake wametoa wito kwa ulimwengu kusaidia kumaliza mgogoro huo na kuishutumu Marekani kwa kuzuia kufikiwa utatuzi.
-
Yemen yaionya Israel, Marekani: Tunaitazama Gaza; vidole vyetu viko kwenye kitufe cha bunduki
Mar 03, 2025 12:07Harakati ya Ansarullah nchini Yemen imetoa onyo kali dhidi uvamizi wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel unaoungwa mkono na Marekani katika Ukanda wa Gaza, na kusema imejiandaa kikamilifu kuchukua hatua dhidi ya maslahi ya Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.
-
OIC: Mzingiro dhidi ya Gaza ni jinai dhidi ya binadamu
Mar 03, 2025 11:07Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetaja mzingiro wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Gaza kuwa ni jinai dhidi ya binadamu.
-
Misri, Saudia zalaani Israel kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza
Mar 03, 2025 03:37Hatua ya Israel ya kuzuia kuingizwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imelaaniwa na Misri na Saudi Arabia, huku nchi mbili hizo zikisisitiza kuwa kitendo hicho ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
Hamas yasisitiza kutekelezwa usitishaji vita kamili
Mar 03, 2025 02:29Mahmoud al Mardawi mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa abadan harakati hiyo haitakubali kuongezwa muda wa marhala ya kwanza ya makubaliano ya usitishaji vita.
-
Misri: Amani haitapatikana pasi na kuundwa nchi huru ya Palestina
Mar 02, 2025 22:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema kuwa, hakutakuwa na usalama katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) bila ya kuasisiwa taifa la Palestina.
-
Mamlaka ya Ndani ya Palestina yataka walimwengu waishinikize Israel
Mar 02, 2025 22:53Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeonya juu ya matokeo mabaya ya kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza na kuitaka jamii ya kimataifa kuulazimisha utawala wa Kizayuni utekeleze majukumu yake ya kibinadamu.
-
Yemen yaitaka Riyadh ijifunze kutokana na hatma ya Zelensky
Mar 02, 2025 08:55Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amewaonya maafisa wa Saudi Arabia na kuwataka wapate somo na ibra kutokana na jinsi Marekani ilivyomfanyia Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na kuwaonya dhidi ya kuitegemea kipofu Washington.