Hamas yasisitiza kutekelezwa usitishaji vita kamili
Mahmoud al Mardawi mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa abadan harakati hiyo haitakubali kuongezwa muda wa marhala ya kwanza ya makubaliano ya usitishaji vita.
Amesema, Hamas inafuatilia kutekeleza marhala zote za makubaliano hayo kwa mujibu wa kile kilichosainiwa.
Mahmoud al Mardawi amesisitiza kuwa Wazayuni maghasibu watawapata mateka wao kupitia makubaliano ya kubadilishana wafungwa. Mardawi ameongeza kuwa, hii ni katika hali ambayo Netanyahu anajidanganya kwamba anaweza kufidia kufeli kwake vitani kwa kuwasababishia njaa ya wananchi wa Palestina na kuwa anaweza kufikia malengo yake kupitia njia hiyo.
Kiongozi huyo wa Hamas ameendelea kubainisha kuwa: Hakuna furs anyingine ya kuketi kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya kuwarejesha mateka na pande suhuhishi zinapasa kuishinikiza Israel kutekeleza kikamilifu makubaliano ya kusimamisha vita.
Mardawi amesema, Misri imeieleza Hamas mara kadhaa kwamba inapinga mipango ya kuwafukuza Gaza Wapalestina na inalitambua suala hilo kuwa linahusiana na usalama wa taifa la Palestina na kwamba inaunga mkono haki za wananchi wa Palestina.