Pars Today
Kwa mujibu wa uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel ndani ya jamii ya Wazayuni, asilimia 61 miongoni mwao wanaamini kuwa utawala huo haujapata ushindi katika vita dhidi ya Hizbullah ya Lebanon.
Zambia imetia saini Hati ya Makubaliano (MOU) na China ya ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha utengenezaji chanjo ya kipindupindu nchini humo na barani Afrika pia.
Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema harakati hiyo ya muqawama haitaafiki makubaliano ambayo yanahalalisha uwepo wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa, Tehran inaunga mkono makubaliano na uamuzi wowote wa makundi ya muqawama na wananchi wa Palestina.
Baraza la mawaziri la vita la utawala wa Kizayuni wa Israel limeidhinisha kuendelea kuwepo kwa jeshi katika Ukanda wa Philadelphi kwenye mpaka wa pamoja wa Ukanda wa Ghaza na Misri na hivyo kudidimiza matumaini ya kusitishwa na hatimaye kukomeshwa vita vya kinyama vilivyoanzishwa na utawala huo dhidi ya eneo hilo tangu Oktoba 7, 2023.
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema utawala ghasibu wa Kizayuni umethibitisha kuwa hautaki kufikia makubaliano; na kwa sababu hiyo, harakati hiyo imewataka wapatanishi wa Misri na Qatar wawalazimishe Wazayuni watekeleze pendekezo la hivi karibuni la usitishaji vita badala ya kutaka yaanzishwe mazungumzo mengine mapya.
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amelaani shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina waliokuwa katika Swala ya Alfajiri katika shule ya al-Tabi’in katika mji wa Gaza.
Mkutano wa pande tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Jordan na Ufaransa ulifanyika Jumamosi Cairo, mji mkuu wa Misri, kuhusiana na matukio ya hivi karibuni katika vita vya Gaza na mashauriano ya kusitisha mapigano hayo.
Mamia ya maelfu ya watu jana waliandamana katika barabara za miji mikuu ya nchi mbalimbali za Ulayakwa wakitaka kusitishwa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza haraka iwezekanavyo; huku idadi ya vifo katika eneo hilo ikipindukia 30,000 kufuatia mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7 mwaka jana.
Maaskofu wa Kanisa la Uingereza wametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano katika eneo la Ukanda wa Gaza. Wito huo umetolewa kabla ya shambulio la anga la jeshi la Israel lililosababisha mauaji ya halaiki huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.