-
China kusaidia ujenzi wa kiwanda cha kwanza Afrika cha chanjo ya kipindupindu nchini Zambia
Oct 09, 2024 02:26Zambia imetia saini Hati ya Makubaliano (MOU) na China ya ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha utengenezaji chanjo ya kipindupindu nchini humo na barani Afrika pia.
-
Hamas yapinga makubaliano yanayotambua rasmi uwepo wa Israel huko Ghaza
Sep 06, 2024 07:26Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema harakati hiyo ya muqawama haitaafiki makubaliano ambayo yanahalalisha uwepo wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.
-
Kuunga mkono Iran maamuzi ya wananchi na muqawama wa Palestina
Sep 04, 2024 12:41Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa, Tehran inaunga mkono makubaliano na uamuzi wowote wa makundi ya muqawama na wananchi wa Palestina.
-
Israel yaidhinisha jeshi libaki kwenye Ukanda wa Philadelphi na kuua matumaini ya kusitishwa vita
Aug 30, 2024 10:15Baraza la mawaziri la vita la utawala wa Kizayuni wa Israel limeidhinisha kuendelea kuwepo kwa jeshi katika Ukanda wa Philadelphi kwenye mpaka wa pamoja wa Ukanda wa Ghaza na Misri na hivyo kudidimiza matumaini ya kusitishwa na hatimaye kukomeshwa vita vya kinyama vilivyoanzishwa na utawala huo dhidi ya eneo hilo tangu Oktoba 7, 2023.
-
HAMAS: Badala ya mazungumzo mapya, Wazayuni walazimishwe kutekeleza usitishaji vita
Aug 13, 2024 05:40Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema utawala ghasibu wa Kizayuni umethibitisha kuwa hautaki kufikia makubaliano; na kwa sababu hiyo, harakati hiyo imewataka wapatanishi wa Misri na Qatar wawalazimishe Wazayuni watekeleze pendekezo la hivi karibuni la usitishaji vita badala ya kutaka yaanzishwe mazungumzo mengine mapya.
-
Borrell: Mauaji ya umati ya Israel Ukanda wa Gaza hayawezi kutetewa
Aug 11, 2024 11:22Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amelaani shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina waliokuwa katika Swala ya Alfajiri katika shule ya al-Tabi’in katika mji wa Gaza.
-
Ufaransa, Misri na Jordan zapinga shambulio la Rafah na kuunga mkono usitishaji vita Gaza
Apr 01, 2024 02:17Mkutano wa pande tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Jordan na Ufaransa ulifanyika Jumamosi Cairo, mji mkuu wa Misri, kuhusiana na matukio ya hivi karibuni katika vita vya Gaza na mashauriano ya kusitisha mapigano hayo.
-
Mamia ya maelfu waandamana barani Ulaya wakitaka kusitishwa vita Gaza
Mar 04, 2024 02:29Mamia ya maelfu ya watu jana waliandamana katika barabara za miji mikuu ya nchi mbalimbali za Ulayakwa wakitaka kusitishwa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza haraka iwezekanavyo; huku idadi ya vifo katika eneo hilo ikipindukia 30,000 kufuatia mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7 mwaka jana.
-
Maaskofu wa Kanisa la Uingereza watoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja huko Gaza
Feb 15, 2024 03:03Maaskofu wa Kanisa la Uingereza wametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano katika eneo la Ukanda wa Gaza. Wito huo umetolewa kabla ya shambulio la anga la jeshi la Israel lililosababisha mauaji ya halaiki huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
HAMAS: Hakutafikiwa makubaliano bila ya kusimamishwa vita na jeshi la Kizayuni kuondoka Gaza
Feb 02, 2024 14:12Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa mjibizo kwa mpango uliopendekezwa wa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza na kutangaza kwamba, hakutafikiwa makubaliano bila ya kusimamishwa vita na jeshi la utawala wa Kizayuni kuondoka Gaza.