Hatimaye makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza yameanza kutekelezwa
(last modified Sun, 19 Jan 2025 13:07:28 GMT )
Jan 19, 2025 13:07 UTC
  • Hatimaye makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Ghaza yameanza kutekelezwa

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kuwa makubaliano ya kusitisha vita katika Ukanda wa Ghaza yameanza kutekelezwa.

Baada ya ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji vita uliofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza leo Jumapili kuwa makubaliano ya usitishaji vita yameingia katika awamu ya utekelezaji.
 
Hapo awali usitishaji vita huo ilipangwa uanze kutekelezwa saa mbili na nusu asubuhi kwa saa za Ghaza, lakini utawala wa Kizayuni uliendeleza mashambulizi yake katika eneo hilo na kuwaua shahidi watu wasiopungua 19 na kuwajeruhi wengine 36.
 
Chaneli ya12 ya televisheni ya Israel nayo pia imeripoti kuwa, jeshi la utawala huo ghasibu limepokea amri ya kusitishwa mapigano huko Ghaza na agizo la kukabidhiwa mateka watatu wa Kizayuni watakaoachiliwa huru na Hamas.
 
Kwa mujibu wa Abu Ubaidah, msemaji wa Brigedi za Al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, mateka watatu wa Waisrael wataachiliwa leo ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kubadilishana mateka ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
 
Jumatano, Januari 15, 2025, Serikali ya Qatar ilitangaza kupatikana mafanikio ya juhudi za kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Ghaza kati ya pande za Palestina na Israel, na kwamba utekelezaji wa makubaliano hayo utaanza kutekelezwa leo (Jumapili, Januari 19) ili kuhitimisha miezi zaidi ya15 ya vita vya kinyama na mauaji ya kimbari ya zaidi ya watu 46,000 yaliyofanywa na jeshi la Kizayuni.../