-
Jihadul Islami yaiambia Israel: Subirini jibu letu kwa mauaji ya mshauri wa IRGC
Dec 26, 2023 23:24Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina sanjari na kulaani mauaji ya Kamanda Sayyid Razi Mousavi, aliyekuwa mshauri wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni unapasa kusubiri jibu kali na zito kwa kitendo chake hicho cha kioga.
-
Israel yashambulia makao makuu ya Hilali Nyekundu Gaza
Dec 26, 2023 23:23Vikosi vya jeshi katili la utawala haramu wa Israel vimeshambulia kwa mabomu makao makuu ya Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Baghdad: Mashambulizi ya US yamekiuka mamlaka ya kujitawala Iraq
Dec 26, 2023 23:23Serikali ya Baghdad imelaani vikali mashambulizi dhidi ya kambi tatu za Harakati ya Kataib Hizbullah nchini Iraq yaliyofanywa na vikosi vamizi vya Marekani kwa amri ya Rais Joe Biden na kueleza kuwa, hujuma hizo hazikubaliki na zimekiuka mamlaka ya kujitawala Iraq.
-
Mpango wa amani wa Yemen kusainiwa mwezi ujao nchini Saudia
Dec 26, 2023 23:23Mpango wa amani wa Yemen unatazamiwa kusainiwa mwanzoni mwa mwezi ujao wa Januari, 2024 nchini Saudi Arabia.
-
Ndege za kivita za Marekani zashambulia makao makuu ya vikosi vya Iraq katika mkoa wa Babel
Dec 26, 2023 08:18Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa, vikosi vamizi vya Marekani leo asubuhi vimekiuka mamlaka ya kujitawala Iraq na kushambulia makao makuu kadhaa ya wapiganaji wa harakati ya Al Hashd al Shaabi huko katikati ya mkoa wa Babel, kusini mwa Baghdad na kujeruhi askari 18 wa Iraq.
-
Ujumbe wa kuendelea maandamano ya wananchi wa Uturuki dhidi ya Israel
Dec 26, 2023 04:02Licha za siasa za kundumakuwili za serikali ya Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki kuhusu masuala ya Palestina, wananchi wa nchi hiyo bado wanaendelea na maandamano yao ya kihamasa dhidi ya Israeli.
-
Makumi ya wanajeshi wa Kizayuni waangamizwa na kujeruhiwa kaskazini mwa Gaza
Dec 26, 2023 03:09Wanajeshi 40 wa Kizayuni wameangamizwa au kujeruhiwa katika operesheni iliyotekelezwa jana Jumatatu na Brigedi za Izzuddinul Qassam tawi la kijeshi la Hamas huko Jabalia, kaskazini mwa Ghaza.
-
Viongozi wa Kizayuni waingiwa na wasiwasi na kiwewe wakihofia jibu la Iran kwa mauaji ya Kamanda Sayyid Razi
Dec 26, 2023 02:40Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa viongozi wa utawala haramu wa Israel wana wasi wasi na hofu kubwa juu ya jibu ambalo Iran itatoa kwa mauaji ya Kamanda Sayyid Razi Mousavi, mshauri wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
-
HAMAS: Wananchi wa Palestina wanataka kukomeshwa kikamilifu uvamizi wa utawala wa Kizayuni
Dec 26, 2023 02:40Izzat al-Rishq, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS amesema: wananchi wa Palestina wanataka kukomeshwa na kuhitimishwa uvamizi wa maghasibu wa Kizayuni na si usitishaji vita wa muda ambapo baada ya muda fulani uvamizi na vitendo vya kigaidi vya maghasibu hao vinaanza kwa mara nyingine tena.
-
UN: Wanawake wawili Wapalestina wanauawa kila saa katika vita vya Israel dhidi ya Gaza
Dec 25, 2023 23:20Wanawake wawili wa Kipalestina wanauawa kila saa moja katika Ukanda wa Gaza katika vita vya maangamizi ya umati vya utawala wa Israel dhidi ya eneo hilo lililozingirwa.