-
Ripoti: Netanyahu hakuenda Davos kutokana na hofu ya kukamatwa
Jan 24, 2026 04:26Vyombo vya habari vya utawala wa Israel vimeripoti kwamba Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, hakuhudhuria Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) mjini Davos wiki hii kutokana na wasiwasi kwamba angeweza kukamatwa nchini Uswisi kufuatia hati ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
-
Hizbullah: Vitisho vya US dhidi ya Kiongozi Muadhamu vitateketeza eneo lote
Jan 24, 2026 00:01Tawi la Kisiasa la Harakati ya Muqawama ya Hizbullah katika Bunge la Lebanon limeonya kwamba, vitisho vya maneno vya Marekani dhidi ya Iran na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei vinaweza kushadidisha mvutano katika eneo la Asia Magharibi.
-
Umoja wa Mataifa: Walowezi wa Kizayuni wamewaua Wapalestina 240 Ukingo wa Magharibi
Jan 23, 2026 10:16Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza katika ripoti yake kwamba mwaka jana (2025) walowezi na jeshi la Israel waliua Wapalestina 240 katika Ukingo wa Magharibi.
-
Abdul-Malik Al-Houthi: Baraza la Amani la Trump ni kifuniko tu cha satwa na uporaji
Jan 23, 2026 04:06Sayyed Abdul Malik al-Houthi, kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, baadhi ya nchi zinaweka mashinikizo makubwa ya kiuchumi kwa watu wa Yemen kwa kuchelewesha kwa makusudi kuwasili meli na kubainisha kwamba Baraza la Amani la Trump ni kifuniko tu cha satwa na uporaji.
-
Tovuti ya Israel: Ujerumani inaendelea kufadhili mauaji ya kimbari huko Gaza
Jan 22, 2026 23:52Tovuti ya Israel, 972+ imechapisha ripoti ndefu ya uchunguzi kuhusu uhusiano wa kijeshi kati ya Ujerumani na Israel, ikihitimisha kwamba mauzo ya silaha ya Ujerumani yameendelea kumiminika Israel licha ya madai kwamba yamesitishwa kutokana na mauaji ya kimbari ya watu wa Gaza.
-
Muqawama wa Yemen na ufafanuzi mpya wa mlingano wa nguvu katika Bahari Nyekundu
Jan 22, 2026 08:11Vyombo vya habari vya utawala ghasibu wa Israel sanjari na kuchapisha ripoti mbalimbali, vimekiri juu ya taathira ya operesheni za vikosi vya muqawama vya Yemen kwa uchumi wa utawala huo.
-
Wakulima Israel wanafilisika baada ya kuongezeka wimbi la kususia bidhaa za kilimo za Israel
Jan 21, 2026 23:37Wakulima wa Israel wameonya kuhusu "kuporomoka kwa mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo kufuatia kuongezeka kwa kampeni za kimataifa za kususia bidhaa za Israel kutokana na vita vya Gaza.
-
B’Tselem: Wapalestina wasiopungua 84 wameuawa kwenye kambi za mateso za Israel
Jan 21, 2026 07:09Mfumo wa magereza wa utawala wa kizayuni wa Israel umekuwa "mtandao wa kambi za mateso" unaowalenga Wapalestina. Hayo yameelezwa katika ripoti mpya ya uchunguzi uliofanywa na asasi ya kutetea haki za binadamu ya B'Tselem.
-
Katibu Mkuu wa UN alaani vikali hatua ya Israel ya kubomoa majengo ya UNRWA Quds Mashariki
Jan 21, 2026 07:07Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani kitendo cha vikosi vya utawala wa kizayuni wa Israel cha kubomoa majengo yaliyomo ndani ya eneo la makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) katika mji wa Baitul Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu.
-
Mauaji ya kimbari ya sekta ya elimu huko Gaza: Walimu zaidi ya elfu moja wameuawa, sekta ya elimu imefungwa
Jan 20, 2026 07:38Ripoti ya pamoja ya Wizara ya Elimu na Elimu ya Juu ya Palestina imeripoti kuwa, kuanzia Oktoba 2023 hadi Oktoba 2025, walimu 1,377 na wafanyakazi wa elimu waliuawa shahidi na 4,757 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya kikatili ya Israel huko Gaza.