-
Amir Abdollahian nchini Lebanon; safari yenye malengo kadhaa
Nov 25, 2023 02:54Hossein Amirabdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametembelea Beirut, mji mkuu wa Lebanon ikiwa ni katika muendelezo wa mashauriano yake na viongozi wa eneo kuhusu hujuma ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza ambapo amekukutana na kuzungumza na maafisa wa nchi hiyo pamoja na viongozi wa mrengo wa muqawama wa Lebanon na Palestina.
-
Kiongozi wa Hamas: Wapalestina wameilazimisha Israel kusitisha mapigano
Nov 25, 2023 01:17Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, amesema Wapalestina wameulazimisha utawala wa Kizayuni wa Israel kukubali masharti ya kundi hilo katika mapatano ya kusitisha mapigano huku akiapa kuwa wapiganaji wa Hamas wataendelea kupigania ukombozi wa Palestina.
-
Abu Ubaida atangaza baadhi ya hasara za Israel katika Kimbunga cha al Aqsa
Nov 25, 2023 01:05Msemaji wa Brigedi za Izzuddin al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), ametangaza kwamba zana na ala 335 za jeshi la Israel zimeharibiwa kabisa tangu kuanza mashambulizi ya utawala huo haramu dhidi ya watu wa Gaza na kusisitiza kuwa, utawala vamizi umelazimika kukubali suluhu na kusitisha mapigano.
-
Waandishi habari wa BBC wawasilisha barua ya malalamiko kuhusu upendeleo na uongo wa shirika hilo katika vita vya Gaza
Nov 25, 2023 01:04Baadhi ya waandishi wa habari wa BBC wamekishutumu chombo hicho cha habari cha serikali ya Uingereza kwa kutangaza uongo na kwa upendeleo kuhusu vita na mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.
-
Sisitizo la China la ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kukomeshwa vita vya Gaza
Nov 25, 2023 01:03Katika hotuba yake kwenye mkutano wa dharura wa nchi wanachama wa BRICS, Rais Xi Jinping wa China amesema kuwa jamii ya kimataifa haipasi kuruhusu mzozo wa Palestina na Israel kuongezeka na kuathiri eneo zima la Mashariki ya Kati, yaani Asia Magharibi.
-
Malori ya misaada yaingia Gaza baada ya kuanza kutekelezwa usitishajii vita wa siku nne
Nov 24, 2023 08:11Msemaji wa kivuko cha Rafah kati ya Ukanda wa Gaza na Misri ametangaza kuwa, malori yaliyobeba misaada ya kibinadamu na mafuta yameanza kuingia kwenye ukanda huo na inatarajiwa kwamba malori 230 yataingia eneo hilo linalokabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.
-
Usitishaji vita wa muda Gaza waanza kutekelezwa
Nov 24, 2023 04:45Usitishaji vita wa siku 4 huko Ukanda Gaza umetekelezwa katika siku ya 49 ya vita kati ya Hamas na utawala wa Kizayuni.
-
Hali si hali kwa wanajeshi wa Israel Ghaza, wakimbia, waadhibiwa
Nov 23, 2023 23:22Duru za habari za Kizayuni zimefichua kuwa, hali si hali kwa wanajeshi wa Israel katika vita vya Ghaza kiasi kwamba jeshi la utawala wa Kizayuni limelazimika kuweka adhabu kali sana kutokana na kuongezeka idadi ya wanajeshi wa Israel wanaokimbia vitani kwa woga na kiwewe kilichowapata.
-
Hizbullah yaendelea kuishambulia Israel, yaangamiza idadi kubwa ya wanajeshi Wazayuni
Nov 23, 2023 23:21Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon jana Alkhamisi ilitoa taarifa 10 za mfululizo na kutangaza kuwa, imeyapiga kwa makombora maeneo hassas na muhimu ya adui Mzayuni na kuangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa Israel.
-
Mchambuzi Mzayuni: HAMAS wamejipanga vizuri kwa vita, tofauti na Israel
Nov 23, 2023 23:21Mchambuzi mmoja Mzayuni amesema kuwa, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imejipanga vizuri na inaendesha kwa umahiri wa hali ya juu vita vya Ghaza, tofauti na Israel ambayo malengo yake hasa, hayajulikani na haifahamiki inaendesha vita vya Ghaza kwa mikakati gani.