-
Sayyid Hassan Nasrullah: Hakuna tena mamlaka ya kiamri ya Marekani duniani
May 26, 2023 03:30Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema hakuna tena mamlaka ya kiamri ya Marekani duniani na kila kitu kinaelekea kwenye ulimwengu wa kambi kadhaa, na akaongezea kwa kusema: "na hili ndilo linaloitia wasiwasi Israel".
-
Marekani inapanga kujenga kituo cha pili cha kijeshi magharibi ya Iraq
May 26, 2023 03:12Duru moja ya masuala ya usalama ya Iraq imefichua kuwa wanajeshi magaidi wa Marekani wanapanga kujenga kambi mpya ya kijeshi katika mkoa wa al-Anbar ulioko magharibi mwa Iraq.
-
China yaitaka Israel iache chokochoko, uporaji wa ardhi za Wapalestina
May 25, 2023 23:50China imeutaka utawala haramu wa Israel ukomeshe mara moja tabia yake ya uchokozi, kuchochea taharuki na kupora ardhi na rasilimali za Wapalestina hasa katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Wazayuni: Ni muujiza tu ndio utatuokoa mbele ya operesheni za Wapalestina Ukingo wa Magharibi
May 25, 2023 06:07Kituo cha upashaji habari cha "al Mu'uti" cha Palestina kimetangaza kuwa, wanamapambano wa Palestina wamefanya operesheni 25 dhidi ya walowezi wa Kizayuni katika kipindi cha masaa 24 ya hadi ilipotangazwa habari hiyo na kuwakosesha usingizi kabisa walowezi hao ambao wanasema waziwazi kuwa ni muujiza tu ndio utaokoa maisha yao.
-
Utunishaji misuli wa Hizbullah na sisitizo la kuwepo umoja katika nyuga zote za Muqawama
May 25, 2023 07:57Jumapili ya tarehe 21 Mei, sambamba na kuwadia maadhimisho ya mwaka wa 23 wa kukombolewa eneo la kusini mwa Lebanon, harakati ya Muqawama ya Hizbullah ilifanya mazoezi makubwa ya kijeshi kwa lengo la kuonyesha utayarifu wa muqawama wa kuilinda ardhi ya Lebanon.
-
Azimio la WHO: Tel Aviv idhamini afya ya Wapalestina
May 25, 2023 02:56Shirika la Afya Duniani (WHO) jana lilipasisha azimio kuhusu hali ya kiafya huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na wajibu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umetakiwa kudhamini afya ya raia wa Palestina.
-
Unicef yaonya kuhusu tishio la njaa kwa watoto wa Yemen
May 25, 2023 02:49Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kuwa mamilioni ya watoto huko Yemen wamebakiza hatua moja tu kukumbwa na njaa.
-
Wayemen wafanya maandamano makubwa katika Siku ya Kupambana na Uistikbari
May 24, 2023 07:25Wananchi wa Yemen leo Jumatano wamekusanyika katika maidani kuu ya mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a na katika miji mingine ya nchi hiyo kufanya maandamano makubwa kwa mnasaba wa Siku ya Kupambanan na Uistikbari yaani "Yaum Sarkha."
-
HAMAS yawaonya Wazayuni wasitoe vitisho dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
May 24, 2023 02:05Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameuonya utawala wa Kizayuni usitoe vitisho dhidi ya Iran akisisitiza kuwa, vitisho hivyo vya Israel dhidi ya nchi za kambi ya muqawama, vinaonesha hofu na kiwewe ilicho nacho Tel Aviv kutokana na nguvu za wanamapambano wa kambi ya muqawama katika kona zote za ukanda huu.
-
Mohammed bin Salman wa Saudia akataa kukutana na Netanyahu
May 23, 2023 22:28Duru za kidiplomasia za kigeni zinasema kuwa hakuna maendeleo yoyote katika kuanzishwa uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia kati ya utawala haramu wa Israel na Saudi Arabia, kwani Mrithi wa Ufalme wa Saudia Mohammed bin Salman (MBS) amekataa ombi la waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu la kukutana naye.