-
Wapalestina walaani safari ya rais wa Israel nchini Uturuki
Mar 10, 2022 04:31Harakati za mapambano ya Kiislamu ambazo zinapigania ukombozi wa Palestina zimelaani vikali safari ya rais wa utawala haramu wa Israel Isaac Herzog nchini Uturuki wakati huu ambao Israel imeshadidisha hujuma dhidi ya Wapalestina.
-
Waturuki wachoma moto bendera za Wazayuni kulaani safari ya Rais wa Israel
Mar 10, 2022 00:40Wananchi wa Uturuki wamefanya maandamano makubwa ya kupinga na kulaani safari ya Isaac Herzog, rais wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel nchini humo.
-
Mazungumzo baina ya Iran na Oman kuhusu usalama wa baharini
Mar 10, 2022 00:40Kikao cha Tatu cha Makamanda wa Gadi ya Ufukweni ya Jamhuri ya Kiisalmu ya Iran na Oman kimefanyika mjini Muscat na kujadili usalama wa baharini. Maudhui kuu iliyojadiliwa na nchi hizi mbili ndugu katika kikao hicho ni kuzidi kushirikiana na kuwa na uratibu wa pamoja na kulinda usalama wa mpaka wa baharini wa nchi hizo.
-
Imarati inawajengea vitongoji askari wa Israel huko Socotra, Yemen
Mar 09, 2022 07:12Umoja wa Falme za Kiarabu umeripotiwa kujenga vitongoji katika kisiwa cha kistratijia cha Yemen cha Socotra ambacho kinakaliwa kwa mabavu na Imarati, kwa ajili wanajeshi wa utawala haramu wa Israel; zaidi ya mwaka mmoja baada ya tawala hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kawaida.
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Ni ujuha na ujinga kuiamini Marekani
Mar 09, 2022 01:09Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani imetenda jinai nyingi dhidi ya wananchi wa mataifa mbalimbali ya dunia na kuiamini nchi hiyo ni ujuha na ujinga.
-
Njama mpya ya Israel ya kuuyahidisha mji mtakatifu wa Quds
Mar 09, 2022 01:07Utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kujenga kituo kikubwa cha Kiyahudi katika eneo la Jabal Zaytun mashariki mwa mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
-
Wananchi wa Yemen waandamana dhidi ya wahusika wa maafa ya kibinadamu nchini humo
Mar 08, 2022 23:07Huku vita na mzingiro vikiendelea dhidi ya taifa la Yemen katika hali ambayo jamii ya kimataifa imekaa kimya, wananchi wa nchi hiyo kwa mara nyingine wamefanya maandamano ya kupinga vita na kuutaja muungano wa Saudia, Umoja wa Mataifa na madola ya Magharibi kuwa wahusika wakuu wa maafa ya kibinadamu yanayoendelea nchini humo.
-
Makumi ya wanawake wa Yemen ni wahanga wa mabomu ya vishada ya Saudi Arabia
Mar 09, 2022 04:03Mabomu ya vishada ambayo yamekuwa yakimiminiwa wananchi wasio na hatia wa Yemen na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia yamepelekea kwa akali wanawake 115 kuuawa shahidi na kujeruhiwa.
-
Wanawake 60 wauawa shahidi Ghaza katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita
Mar 08, 2022 07:03Kituo cha Haki za Binadamu cha Mizan kimetoa ripoti kwa mnasaba wa Siku ya Mwanamke Ulimwenguni na kusema kuwa, wanawake 60 wa Palestina wameuliwa shahidi katika mashambulizi ya Wazayuni huko Ghaza baina ya tarehe 8 Machi 2021 hadi tarehe 8 Machi 2022.
-
Harakati ya Fat'h: Viongozi wa utawala wa Kizayuni wanapaswa kuwajibishwa kwa jinai zao
Mar 08, 2022 04:48Harakati ya Fat'h huko Palestina imeitaka jamii ya kimataifa kuwafikisha mbele ya sheria viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mahakama za kimataifa kutokana na jinai na uhalifu unaofanyika dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.