Njama mpya ya Israel ya kuuyahidisha mji mtakatifu wa Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81174-njama_mpya_ya_israel_ya_kuuyahidisha_mji_mtakatifu_wa_quds
Utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kujenga kituo kikubwa cha Kiyahudi katika eneo la Jabal Zaytun mashariki mwa mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 09, 2022 01:07 UTC
  • Njama mpya ya Israel ya kuuyahidisha mji mtakatifu wa Quds

Utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kujenga kituo kikubwa cha Kiyahudi katika eneo la Jabal Zaytun mashariki mwa mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Aidha utawala wa Kizayuni unatumia fursa iliyojitokeza ya kimya cha jamii ya kimataifa kuendeleza njama yake ya kuuyahudisha mji wa Quds.

Kwa mujibu wa Kanali ya Saba ya Televisehni ya Kizayuni, baraza la mawaziri la utawala huo limeafiki kujengwa kituo kikubwa cha Kiyahudi katika Jabal Zaytun.

Ripoti hiyo imedokeza kuwa kituo hicho kitajumuisha sinagogi, chuo, maktaba, ukumbi wa mikutano, kitengo cha utafiti maalumu na makaburi. Utawala  wa Kizayuni pia katika miezi ya hivi karibuni umekuwa ukitekeleza miradi ya kujenga vitongoji zaidi vya walowezi wa Kizayuni.

Katika miongo ya karibuni, utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel umechukua hatua nyingi kwa lengo la kuubadilisha utambulisho wa Kiislamu wa Quds tukufu, mojawapo ikiwa ni sheria ya kupiga marufuku kusomwa adhana kwa kutumia vipaza sauti katika misikiti ya mji huo.

Vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni

Desemba 23, 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio 2334 ambalo liliutaka utawala haramu wa Israel usimamishe haraka na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyahudisha maeneo hayo, kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.