-
Syria yalaani hujuma ya Israel dhidi ya Damascus
Feb 10, 2022 07:20Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imelaani vikali mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala haramu wa Israel dhidi ya maeneo ya Syria ambayo yamesababisha vifo na kujeruhi idadi kadhaa ya wanajeshi wa Syria.
-
Jeshi la Yemen latungua ndege ya kijasusi katika mkoa wa Hajjah
Feb 10, 2022 07:07Vikosi vya Yemen vimefanikiwa kudungua ndege isiyo na rubani ya kijasusi ya muungano wa wavamizi unaoongozwa na Saudi Arabia katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Hajjah.
-
PLO yasimamisha uamuzi wa kuutambua utawala wa Kizayuni wa Israel
Feb 10, 2022 04:05Baraza Kuu la Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO limetangaza kuwa limesimamisha uamuzi wa kuutambua utawala haramu wa Kizayuni wa Israel pamoja na ushirikiano wa kiusalama na utawala huo.
-
Kiongozi wa Hamas: Imam Khomeini alifanikiwa kuwafanya wananchi wa Iran waiunge mkono Palestina
Feb 09, 2022 23:32Ismail Ridhwan, kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Imam Ruhullah Khomeini (MA) muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alifanikiwa kuwageuza wananchi wa Iran na kuwafanya waiunge mkono kadhia ya Palestina.
-
Mandela: Tofauti baina ya utawala wa zamani Afrika Kusini (apartheid) na Israel ni katika ukubwa wa unyama na ukatili
Feb 09, 2022 23:31Mjukuu wa hayati mzee Nelson Mandela amesema kuwa, tofauti baina ya utawala wa zamani wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini (apartheid) na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ni katika ukubwa na ukatili wake.
-
Guterres: Ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni changamoto kwa usalama wa dunia
Feb 09, 2022 09:57Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, hali ya mambo katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ukiwemo mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) ni changamoto kubwa kwa amani na usalama wa dunia.
-
Vipengee vya kimkakati katika matamshi ya Sayyid Hassan Nasrullah
Feb 09, 2022 07:09Mahojiano maalumu ya televisheni ya Al-Alam na Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah, Jumanne jioni, kuhusu hali ya ndani ya Lebanon na matukio ya kikanda na kimataifa, yamepewa mazingatio katika vyombo vya habari vya kimataifa kutokana na vipengee vya masuala ya kistratijia yaliyojadiliwa katika mahojiano hayo.
-
Oxfam: Mapigano ya Ma'rib yamesababisha raia raia laki moja kuwa wakimbizi
Feb 09, 2022 04:07Shirika la Kimataifa la Misaada kwa ajili ya Kupambana na Umaskini na Njaa (Oxfam) limetangaza kuwa, mapigano ya mwaka mmoja katika mji wa kistratejia wa Ma'rib huko Yemen yamesababisha watu karibu laki moja kuwa wakimbizi.
-
Syria yazuia mashambulio ya Wazayuni dhidi yake
Feb 09, 2022 04:00Vyanzo vya Syria vimeripoti leo alfajiri kwamba mifumo ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo imefanikiwa kuzuia mashambulio yaliyofanywa na utawala ghasibu wa Israel kuulenga mji mkuu wa nchi hiyo Damascus.
-
Nasrullah: Iran ni nguvu kubwa kieneo na yenye taathira kubwa duniani
Feb 09, 2022 03:26Katibu Mkuu wa Chama cha Hizbullah cha nchini Lebanon ameashiria furaha kubwa waliyokuwanayo wananchi wa Iran wakati wa kurejea nchini Imam Khomeini (MA) kutoka uhamishoni na kusema hiyo ni moja ya nukta za kuvutia zaidi katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanayojulikana kama Alfajiri Kumi.