-
Taliban wasema wako tayari kushiriki kwenye serikali ya mpito ya Afghanistan
Aug 12, 2021 21:54Kundi la Taliban limetangaza kuwa liko tayari kushiriki katika serikali ya mpito ya Afghanistan.
-
Maafa ya Yemen na kibarua kizito cha mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa
Aug 12, 2021 21:51Katika kipindi cha sasa ambako hakuonekani ishara yoyote ya kumalizika vita vya Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya watu wa Yemen, Umoja wa Mataifa umemteua Mjumbe wake mpya katika masuala ya nchi hiyo iliyoathiriwa na vita. Hatua hii imetambuliwa na maafisa wa Yemeni kwamba haitakuwa na taathira ya maana katika kukomesha maafa yanayoendela kufanyika nchini humo.
-
UN yataka kusitishwa jinai za Israel dhidi ya wanaharakati wa Palestina
Aug 12, 2021 08:22Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kusitishwa jinai na uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wanaharakati wa Palestina.
-
Ansarullah: Marekani inazuia suhulu ya kisiasa katika mgogoro wa Yemen
Aug 12, 2021 03:36Msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani inakwamisha na kuzuia kupatikana suluhisho la kisiasa katika mgogoro unaoikabili nchi hiyo maskini ya Kiarabu inayozongwa na vita na mapigano tokea mwaka 2015.
-
Jihad Islami ya Palestina yasikitishwa na safari ya waziri wa Israel Morocco
Aug 11, 2021 22:51Msemaji wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amelaani vikali safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel nchini Morocco na kubainisha kuwa, ziara hiyo haikubaliki.
-
Malengo ya Iraq katika kuandaa kikao cha nchi jirani
Aug 11, 2021 21:55Serikali ya Iraq inafanya juhudi za kuandaa kikao cha viongozi wa nchi za eneo na nchi kadhaa za kimataifa kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel awasili Rabat licha ya safari yake kupingwa vikali na Wamorocco
Aug 11, 2021 09:08Duru za habari zimeripoti kuwa licha ya upinzani mkali wa asasi na wanaharakati wa Morocco, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amefanya safari kuelekea nchi hiyo ya Kiarabu iliyoko Afrika Kaskazini.
-
Asa'ib Ahl al-Haq ya Iraq: Tuna haki ya kujibu mashambulio ya Israel
Aug 10, 2021 23:17Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya nchini Iraq amesema kambi hiyo ya muqawama ina haki ya kujibu mapigo, kufuatia mashambulio ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambayo yameua vijana kadhaa wa mrengo huo wa mapambao ya Kiislamu.
-
Wayemen waandamana jijini Sana'a wakitaka kuondolewa mzingiro
Aug 10, 2021 23:15Wananchi wa Yemen jana Jumanne walifanya maandamano nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sana'a, kulaani mzingiro uliowekwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo.
-
Haniya: Tunawashikilia mateka wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel
Aug 10, 2021 07:50Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema maudhui ya mateka wa vita bado iko mezani na kwamba Hamas inawashikilia mateka wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza.