UN yataka kusitishwa jinai za Israel dhidi ya wanaharakati wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i73434-un_yataka_kusitishwa_jinai_za_israel_dhidi_ya_wanaharakati_wa_palestina
Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kusitishwa jinai na uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wanaharakati wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 12, 2021 08:22 UTC
  • Mary Lawlor
    Mary Lawlor

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kusitishwa jinai na uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wanaharakati wa Palestina.

Bi Mary Lawlor ametahadharisha kuhusu jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wanaharakati wa Palestina ikiwa ni pamoja na kutiwa mbaroni kiholela, mateso na vitisho na kusisitiza ulazima wa kukomeshwa vitendo hivyo.

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa amekosoa pia vitendo vya utawala ghasibu wa Israel vya kuwakamata na kuvamia nyumba za wanaharakati wa haki za binadamu wa Kipalestina na kuutaka utawala huo ewaachie huru haraka wanaharakati watatu wa haki za binadamu wa Palestina ambao ni Muna al Kurd, Muhammad al Kurd na Zuhair al Rajabi.  

Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Palestina, Muna al Kurd aliyeko mbaroni 

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ametilia mkazo umuhimu wa kulindwa wanaharakati wa haki za binadamu wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Amesema ana wasiwasi kuhusu hatu ya Israel ya kumtiwa nguvuni Farid al Atrish, mwanaharati wa haki za binadamu wa Palestina ambaye alikamatwa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni katika maandamano ya amani tarehe 15 Juni mwaka huu huko Bait Laham.   

Karibu Wapalestina 4,800 wanashikiliwa katika jela mbalimbali za utawala haramu wa Israel wakiwemo watoto 170,  wanawake 39 na makumi ya wazee.