-
Wabunge wa Misri wataka nchi yao irejeshe uhusiano wake na Syria
Feb 01, 2021 08:28Wabunge wa Misri wamesema kuwa, hakuna kizuizi chochote katika njia ya kuboresha uhusiano wa nchi hiyo na Syria.
-
Wapalestina watungua ndege ya kijasusi ya Israel
Feb 01, 2021 04:49Wanamapambano wa Kiislamu wa Palestina, usiku wa kuamkia leo wametungua ndege moja isiyo na rubani ya utawala wa Kizayuni iliyokuwa ikifanya ujasusi katika anga ya Ukanda wa Ghaza.
-
Al Kadhimi asisitiza kulipiza kisasi kwa wahusika wa milipuko ya Baghdad
Jan 31, 2021 04:04Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kuwa, wale wote walioihusika katika kuwaua raia wasio na hatia katika milipuko ya karibuni katika maidani ya al Tayaran huko Baghdad mji mkuu wa nchi hiyo watalipizwa kisasi.
-
Harakati ya Ansarullah yataka Umoja wa Mataifa ujadili maafa ya Yemen
Jan 30, 2021 09:02Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetoa wito kwa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wajadili hali mbaya ya kibinaadamu nchini Yemen ambayo imetokana na uvamizi wa muungano unaoongozwa na Saudia.
-
Syria yalalamika kuhusu jinai zinazofanywa na magaidi wanaopata himaya ya Marekani
Jan 30, 2021 08:58Syria imesema wanaotenda jinai dhidi ya watoto wa Syria wakiwemo magaidi na wanamgambo wa Kikurdi wa SDF wanapata himaya ya Marekani.
-
Ukosoaji wa kuchelewa wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusu kadhia ya Palestina
Jan 29, 2021 23:14Akizungumza Jumanne katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoandaliwa kwa ajili ya kujadili masuala ya eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) Ahmad Abu al-Ghait, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu au kwa jina jingine Arab League, alisema kuwa Wapalestina wamepitia mashinikizo makubwa yasiyo na mfano wake katika miaka minne ya utawala wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump.
-
Mabaki ya msikiti wa kale yadhihirisha jinsi Uislamu ulivyo na uvumilivu kwa dini zingine
Jan 29, 2021 09:36Wanaakiolojia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel wamesema, wamegundua mabaki ya msikiti wa kale ambao inaaminika ni wa miongo ya tangu mwanzoni mwa Uislamu. Mabaki ya msikiti huo yamegunduliwa katika uchimbuaji uliofanywa katika mji wa Tiberias kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Israel yatoa sharti la kuruhusu chanjo ya corona kuingizwa eneo la Ukanda wa Gaza, Palestina
Jan 29, 2021 09:33Gazeti moja la Kizayuni limeripoti kuwa utawala haramu wa Israel ungali unaweka vizuizi dhidi ya mpango wa kuingiza chanjo ya corona katika eneo la Ukanda wa Gaza na kwamba utawala huo ghasibu umetoa sharti maalumu ili kuruhusu kuingizwa chanjo hiyo katika eneo hilo.
-
Qatar yaishukuru Iran; sisitizo la nafasi chanya ya Iran katika kuleta uthabiti na amani katika eneo
Jan 29, 2021 06:03Huku akisisitiza kuwa uhusiano wa Qatar na nchi mbili za Iran na Uturuki ni mzuri sana, Lolwah al Khater, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar amezishukuru nchi hizo kwa kuwa pembeni ya taifa hilo wakati ilipokuwa chini ya mgogoro mkubwa wa kuzingirwa na majirani zake.
-
Israel yatuhumiwa kuhusika na njama ya kumuua Rais wa Tunisia
Jan 29, 2021 04:02Harakati ya al-Shaab ya Tunisia imesema utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika na njama ya kutaka kumuua Rais Kais Saied wa nchi hiyo kwa kutumia sumu.