Israel yatuhumiwa kuhusika na njama ya kumuua Rais wa Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66224-israel_yatuhumiwa_kuhusika_na_njama_ya_kumuua_rais_wa_tunisia
Harakati ya al-Shaab ya Tunisia imesema utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika na njama ya kutaka kumuua Rais Kais Saied wa nchi hiyo kwa kutumia sumu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 29, 2021 04:02 UTC
  • Israel yatuhumiwa kuhusika na njama ya kumuua Rais wa Tunisia

Harakati ya al-Shaab ya Tunisia imesema utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika na njama ya kutaka kumuua Rais Kais Saied wa nchi hiyo kwa kutumia sumu.

Katibu Mkuu wa harakati hiyo, Zahir al-Maghzavi, ameiambia kanali ya televisheni ya al-Mayadeen ya Lebanon kuwa, huenda utawala ghasibu wa Israel una mkono katika njama hiyo iliyofeli ya kutaka kumuua Rais Kais Saied wa Tunisia.

Amesema nukta inayoupa nguvu uwezekano wa kuhusika Israel katika njama hizo, ni kutokana na msimamo wa Rais huyo wa Tunisia wa kuliuga mkono taifa la Palestina na kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Israel na nchi za Kiarabu.

Siku ya Jumatano, Ofisi ya Rais wa Tunisia ilibainisha katika taarifa kuwa, mtu au watu wasiojulikana walikula njama ya kutaka kumuua Rais Saied kwa kutuma barua iliyotiwa ndani yake mada za sumu. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kais Saied yuko salama usalimini na hajapatwa na hatari yoyote.

Maandamano ya Watunisia ya kupinga uhusiano na Israel

Imeelezwa kuwa ndani ya bahasha ya barua iliyotumwa Ikulu ya Rais wa Tunisia ya Qartaj mlikuwa na mada hatari za sumu.

Hivi karibuni Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Tunisia iliashiria juhudi za baadhi ya mataifa ya kieneo za kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, serikali ya Tunis haina mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.