Wabunge wa Misri wataka nchi yao irejeshe uhusiano wake na Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66350-wabunge_wa_misri_wataka_nchi_yao_irejeshe_uhusiano_wake_na_syria
Wabunge wa Misri wamesema kuwa, hakuna kizuizi chochote katika njia ya kuboresha uhusiano wa nchi hiyo na Syria.
(last modified 2026-08-14T10:24:44+00:00 )
Feb 01, 2021 08:28 UTC
  • Wabunge wa Misri wataka nchi yao irejeshe uhusiano wake na Syria

Wabunge wa Misri wamesema kuwa, hakuna kizuizi chochote katika njia ya kuboresha uhusiano wa nchi hiyo na Syria.

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Misri wamesisitiza kuwa, kuna ulazima wa kuanza tena uhusiano wa kidiplomasia baina ya Cairo na Damascus. Mustafa Bakri mmoja wa Wabunge hao amebainisha kuwa, Syria haijaitia hasara yoyote Misri, bali daima imekuwa ikiitetea Cairo katika vita na ugaidi.

Ameongeza kuwa, jambo linapopaswa kupewa kipaumbele ni Misri kuanzisha tena uhusiano wake na Syria, hasa kwa kutilia maanani kwamba, Cairo imerejesa uhusiano wake wa kawaida na Qatar, licha ya kuwa, Doha kama alivyodai imefanya uhalifu mwingi dhidi ya Cairo.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa, sahihi suala la kuzorota na kukatwa uhusiano wa Misri na Syri liedelee kushuhudiwa.

Rais Bashar al-Assad wa Syria

 

Alaa Isam, Mbunge mwingine wa Misri ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Bunge la Misri amepongeza ushindi wa jeshi la Syria katika vita dhidi ya ugaidi na kutaka nchi yake irejeshe uhusiano wake na nchi hiyo.

Itakumbukwa kuwa kufuatia machafuko yaliyotokana na njama za madola ya Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu zikiongoza na Marekani na Saudi Arabia, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ilisimamisha uanachama wa Syria kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al Assad. Licha ya upinzani mkubwa wa Saudia, lakini nchi nyingi za Kiarabu na kufuatia ushindi mtawalia wa serikali ya Damascus dhidi ya makundi ya kigaidi, hivi sasazimekuwa zikiitaka Arab League kuirejeshea kiti chake Damascus ndani ya jumuiya hiyo.