-
Jihad Islami yalaani Israel kuwazuia Waislamu kuingia Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim
May 29, 2020 23:22Mwanachama wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni ya kuwazuia Waislamu Wapalestina kuingia Msikiti wa Haram ya Nabii Ibrahim mjini al Khalil (Hebron) na kusema kitendo hicho ni hujuma ya wazi.
-
Syria: Umoja wa Ulaya unafuata kidhalili siasa za uadui za Marekani
May 29, 2020 06:17Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeashiria hatua ya Umoja wa Ulaya ya kurefusha vikwazo dhidi ya nchi hiyo na kusema kuwa ni kuifuata Marekani kwa njia ya kujidhalilisha na kwamba pia ni jinai dhidi ya binaadamu.
-
Hali ya kiafya ya kiongozi wa HAMAS anayeshikiliwa katika jela ya Saudia yazidi kuzorota
May 29, 2020 06:07Hali ya kiafya ya Muhammad Khidhri, mwakilishi wa harakati ya muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ambaye alitiwa mbaroni miezi kadhaa iliyopita nchini Saudia, imezidi kuwa mbaya.
-
Uhusiano mzuri wa Iran na Afghanistan katika kivuli cha mawasiliano endelevu
May 29, 2020 04:53Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulika masuala ya sheria amesema kuwa, ili kuzuia magendo ya binaadamu na safari haramu, Tehran imetiliana saini makubaliano mapya na serikali ya Afghanistan.
-
Jihadul Islami: Shahid Soleimani alikuwa na mchango mkubwa sana wa kuimarika muqawama wa Palestina
May 29, 2020 02:09Mwakilishi wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina huko Lebanon amesisitiza kuwa, mchango wa Luteni Jenerali Shahid Qassem Soleimani, Kamanda wa Jeshi la Quds la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni mkubwa sana katika kuimarika muqawama wa makundi ya Paelstina huko Ghaza kiasi kwamba muqawama wa Wapalestina umewashinda Wazayuni na kuzidi kuonesha udhaifu wa utawala pandikizi wa Israel.
-
Jeshi la Iraq lamuua kiongozi wa ISIS nchini Syria
May 29, 2020 01:46Televisheni ya al Mayadeen imeripoti kuwa, kiongozi mmoja mkubwa wa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) ameuawa katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi la Iraq katika maficho ya magaidi hao huko Deir ez-Zor, Syria.
-
Kuongezeka maonyo dhidi ya Israel kuhusu kuunganishwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
May 29, 2020 01:30Katika hali ambayo Benjamini Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel tayari ameainisha taraehe ya kuunganisha Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo (Israel), maonyo yanaendelea kutolewa dhidi ya hatua hiyo hatari.
-
Iraq: Hatuna haja na wageni katika kupambana na magaidi wa ISIS
May 27, 2020 21:53Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Iraq amesema, nchi yake ina uwezo wa kutosha wa kupambana na kuwamaliza magaidi wa Daesh (ISIS) hivyo haina haja na msaada wa wanajeshi kutoka nje.
-
Sayyid Hassan Nasrallah abainisha nafasi ya leo ya harakati ya muqawama
May 27, 2020 21:51Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu MKuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amefanya mahojiano kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 20 wa kukombolewa eneo la kusini mwa Lebanon ambalo lilikuwa limekaliwa kwa mabavu na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel. Jeshi hilo la Kizayuni lililazimika kuondoka kwa madhila kusini mwa Lebanon mnamo Mei 25 mwaka 2000.
-
Uhalifu washtadi Saudia, 6 wauawa katika makabiliano ya risasi
May 27, 2020 09:57Kwa akali watu sita wameuawa katika tukio la ufyatulianaji risasi katika mji wa al-Amwah ulioko katika mkoa wa Assir kusini magharibi mwa Saudi Arabia, mpakani na Yemen.