Syria: Umoja wa Ulaya unafuata kidhalili siasa za uadui za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i61287-syria_umoja_wa_ulaya_unafuata_kidhalili_siasa_za_uadui_za_marekani
Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeashiria hatua ya Umoja wa Ulaya ya kurefusha vikwazo dhidi ya nchi hiyo na kusema kuwa ni kuifuata Marekani kwa njia ya kujidhalilisha na kwamba pia ni jinai dhidi ya binaadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2020 06:17 UTC
  • Syria: Umoja wa Ulaya unafuata kidhalili siasa za uadui za Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imeashiria hatua ya Umoja wa Ulaya ya kurefusha vikwazo dhidi ya nchi hiyo na kusema kuwa ni kuifuata Marekani kwa njia ya kujidhalilisha na kwamba pia ni jinai dhidi ya binaadamu.

Aidha Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria sambamba na kulaani hatua hiyo ya Umoja wa Ulaya imebainisha kwamba EU imekosa uhuru katika maamuzi yake. Itakumbukwa kuwa jana Alkhamisi Umoja wa Ulaya ulitangaza kurefusha vikwazo vyake dhidi ya Syria kwa muda wa mwaka mwingine mmoja. Akisoma taarifa hiyo, Josep Borrell, Mkuu wa Siasa za Nje za umoja huo alisema kuwa vikwazo vya EU dhidi ya Syria vimerefushwa hadi tarehe Mosi Juni 2021 kwa tuhuma kuwa eti serikali ya Damascus inakiuka haki za binaadamu.

Walid al-Muallem, Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria

Hivi sasa watu 273 na taasisi 70 zenye uhusiano na serikali ya Syria zimewekwa katika orodha ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa tuhuma bandia. Tangu mwaka 2011 Umoja wa Ulaya na Marekani ikiwa ni katika fremu ya kuwaunga mkono magaidi, zimekuwa zikiiwekea Syria aina tofauti ya vikwazo. Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 baada ya makundi mengi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Saudi Arabia, Marekani, Israel na washirika wao kuivamia nchi hiyo ya Kiarabu kwa lengo la kubadili mlingano katika eneo la Asia Magharibi. Syria kama nchi mwanachama mkuu wa muqawama, ina nafasi kubwa katika kukabiliana na njama chafu na hatua za uhasama za Marekani, Israel na Saudi Arabia katika eneo.