Iraq: Hatuna haja na wageni katika kupambana na magaidi wa ISIS
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i61253-iraq_hatuna_haja_na_wageni_katika_kupambana_na_magaidi_wa_isis
Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Iraq amesema, nchi yake ina uwezo wa kutosha wa kupambana na kuwamaliza magaidi wa Daesh (ISIS) hivyo haina haja na msaada wa wanajeshi kutoka nje.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 28, 2020 02:23 UTC
  • Iraq: Hatuna haja na wageni katika kupambana na magaidi wa ISIS

Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Iraq amesema, nchi yake ina uwezo wa kutosha wa kupambana na kuwamaliza magaidi wa Daesh (ISIS) hivyo haina haja na msaada wa wanajeshi kutoka nje.

Brigedia Jenerali Yahya Rasoul alisema hayo jana katika mahojiano na televisheni ya al Mayadeen na huku akigusia kwamba magaidi wa Daesh wanatumia mbinu ya mashambulizi ya kushitukiza amesema,  magaidi hao hawana uthubutu wa kukabiliana moja kwa moja na majeshi na vikosi vya ulinzi vya Iraq ambayo vimesimama imara kupambana vilivyo hadi kuwasafisha kabisa magaidi hao nchini humo.

Msemaji huyo wa majeshi ya Iraq pia amesema, nchi yake inabadilishana taarifa za kijasusi na inashirikiana na serikali ya Syria katika kuwaangamiza magaidi wa ISIS.

Brigedia Jenerali Yahya Rasoul 

 

Kwa muda sasa vikosi vya ulinzi vya Iraq vimeanzisha operesheni pana na kubwa ya kupambana na magaidi ili kusafisha mabaki ya wanachama wa genge la ukufurishaji la Daesh (ISIS) lililoanzishwa, kusaidiwa, kupewa mafunzo na kuungwa mkono na madola ya kibeberu ya Magharibi hasa Marekani licha ya madola hayo hivi sasa kujifanya yameanzisha muungano wa kupambana na magaidi hao.

Licha ya magaidi wa Daesh kushindwa huko Iraq, lakini baadhi ya wanachama wa genge hilo wamejificha ndani ya jamii na katika baadhi ya maeneo wakisubiri fursa yoyote ile ili wafanye mashambulio ya kushitukiza kwenye maeneo tofauti ya Iraq.