-
Waziri wa Vita wa Israel aitishia Gaza kwa uharibifu na "tufani kubwa"
Sep 08, 2025 09:13Licha ya kupita takriban miaka miwili tangu kuanza vita dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na kushindwa utawala wa Kizayuni kufikia malengo yake katika vita hivyo, ikiwa ni pamoja na kuiangamiza harakati ya Hamas na kuwakomboa mateka wa Kizayuni wanaoshikiliwa na harakati za mapambano ya ukombozi wa Palestina, Waziri wa Vita wa utawala huo Yisrael Katz, kwa mara nyingine ameitishia harakati ya Hamas kwa "tufani kubwa" huko Gaza.
-
Wazayuni 6 wauawa kwa kupigwa risasi huko Quds (Jerusalem)
Sep 08, 2025 08:54Waisraeli 6 wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio la risasi kwenye makutano ya Ramot katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu, mapema leo Jumatatu.
-
Israel yashambulia kwa mabomu mnara wa 50 wa makazi katika mji wa Gaza
Sep 08, 2025 04:03Utawala wa Israel umeshadidisha mashambulizi yake ya kinyama katika Ukanda wa Gaza kwa kushambulia na kubomoa jengo jingine la mnara wa 50 wa makazi ya Wapalestina katika mji wa Gaza huku ikitekeleza mashambulizi ya nchi kavu kwa lengo la kulikalia kwa mabavu eneo hilo.
-
Save the Children: Kila saa moja mtoto mmoja anauawa shahidi Gaza
Sep 07, 2025 23:03Shirika la Kimataifa la Save the Children limetangaza kuwa, hali ya watoto Gaza ni mbaya mno na kwamba, kila saa moja mtoto mmoja anauawa shahidi katika Ukanda huo unaokabiliwa na mzingiro.
-
Rais wa Lebanon aiomba Marekani kuishinikiza Israel iondoke kusini mwa Lebanon
Sep 07, 2025 08:28Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, ameitaka Washington kuishinikiza Israel ili ikomeshe kukalia kwa mabavu ardhi ya kusini mwa nchi hiyo, akisema hatua hiyo itafungua njia kwa jeshi la Lebanon kuchukua udhibiti kamili wa eneo hilo.
-
Saudia yalitaka Baraza la Usalama lisitishe 'sera za uchokozi' za Israel huko Gaza
Sep 06, 2025 08:05Saudi Arabia imelaani mipango ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ya kuwafurusha kwa nguvu Wapalestina kutoka Gaza, ikilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati na kukomesha "sera za uchokozi" za Tel Aviv dhidi ya wananchi wa Palestina na ardhi yao.
-
Walebanon waandamana Beirut wakipinga kupokoywa silaha Hizbullah
Sep 06, 2025 08:04Wafuasi wa Harakati za Muqawama wa Kiislamu za Lebanon za Hizbullah na makundi mengine ya Muqawama ya nchi hiyo wamefanya maandamano makubwa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Beirut, wakipinga vikali pendekezo la baraza la mawaziri linaloungwa mkono na Marekani na Israel la kuwapokonya silaha wanamuqawama.
-
Mawaziri wa Hizbullah na Amal watoka nje ya kikao cha baraza la mawaziri la Lebanon cha upokonyaji silaha
Sep 06, 2025 02:49Mawaziri wa Harakati za Muqawama wa Kiislamu za Lebanon za Hizbullah na Amal wametoka nje ya kikao cha Baraza la Mawaziri la nchi hiyo kupinga uwepo wa kamanda wa jeshi katika kikao cha serikali cha kujadili upokonyaji silaha za Muqawama.
-
Jeshi la kizayuni laporomosha jengo la ghorofa 12 linalowapa hifadhi mamia ya Wapalestina Ghaza
Sep 05, 2025 23:36Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel siku ya Ijumaa liliripua na kuporomosha jengo la ghorofa 12 la makazi ya raia magharibi mwa Mji wa Ghaza linalowapa hifadhi mamia ya Wapalestina waliolazimika kuyahama makazi yao katika eneo hilo lenye msongamano wa watu na ambalo limekuwa kimbilio la makumi ya maelfu ya Wapalestina.
-
Kiongozi wa Wadruze Syria amshukuru Trump, Israel na EU, asisitizia msimamo wa jamii yao kujitawala
Sep 05, 2025 23:35Kiongozi wa kiroho wa jamii ya Wadruze wa Syria, Hikmat al-Hijri ametoa shukurani kwa Marekani, utawala wa kizayuni wa Israel na nchi za Ulaya, akisisitiza kwamba haki ya kujiamualia mustakabali wao ni haki takatifu inayodhaminiwa na mikataba yote ya kimataifa.