Wazayuni 6 wauawa kwa kupigwa risasi huko Quds (Jerusalem)
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i130564-wazayuni_6_wauawa_kwa_kupigwa_risasi_huko_quds_(jerusalem)
Waisraeli 6 wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio la risasi kwenye makutano ya Ramot katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu, mapema leo Jumatatu.
(last modified 2025-09-08T08:54:59+00:00 )
Sep 08, 2025 08:54 UTC
  • Wazayuni 6 wauawa kwa kupigwa risasi huko Quds (Jerusalem)

Waisraeli 6 wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio la risasi kwenye makutano ya Ramot katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu, mapema leo Jumatatu.

Huduma ya ambulensi imesema kuwa saba kati ya waliojeruhiwa kwa kupigwa risasi wako katika hali mbaya.

Yedioth Ahronoth iliripoti kuwa watano kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya na wengine watano wako mahututi.

Kwa upande wake, polisi ya Israel imesema "imewaua" watu wawili waliotekeleza shambulio kwenye makutano ya Ramot.

Harakati ya Mupambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), harakati ya Jihad Islami na makundi mengine ya mapambano ya ukombozi wa Palestina yamebariki operesheni hiyo na kuitaja kuwa ni jibu kwa jinai na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel.

Kufuatia operesheni hiyo, vikosi vya jeshi la utawala vamizi wa Israel vimefunga milango yote ya kuingia Quds inayokaliwa kwa mabavu na vijiji vya kandokando yake.