-
Baraza la Usalama la UN lajadili ongezeko la mgogoro wa wakimbizi duniani
Apr 29, 2025 08:41Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa idadi ya wakimbizi duniani inaakisii hali halisi ya mambo ya zama hizi.
-
Mark Carney: Canada haitasahau usaliti wa Marekani/ Mahusiano ya zamani yamekwisha
Apr 29, 2025 08:31Waziri Mkuu mteule wa Canada, Mark Carney ametoa ujumbe mzito kwa Marekani, akisema kwamba Ottawa haipaswi "kusahau usaliti wa Washington ambao umeathiri vibaya uhusiano wa kibiashara wa nchi hizo mbili.
-
Kampuni ya Uingereza inaipatia Israel injini za ndege zisizo na rubani (Droni)
Apr 29, 2025 08:27Shirika moja la habari la Uingereza limefichua kuwa kampuni ya uhandisi ya RCV Engines ya Uingereza inasambaza kwa Israel injini za kizazi kipya zaidi cha ndege zisizo na rubani zinazotumika kufanya mauaji huko Palestina.
-
Mbunge wa Marekani awasilisha ibara saba za hoja za kumsaili Trump kwa lengo la kumuuzulu
Apr 29, 2025 03:21Mbunge wa chama cha Democrat katika Bunge la Marekani Shri Thanedar amewasilisha vifungu saba vya hoja ya kumsaili na kumuuzulu rais wa nchi hiyo Donald Trump.
-
Kremlin: Russia inaweza kutoa msaada wa kijeshi kwa Korea Kaskazini 'ikiwa italazimu'
Apr 29, 2025 03:20Ikulu ya Russia, Kremlin imesema nchi hiyo inaweza kutoa msaada wa kijeshi kwa Korea Kaskazini chini ya makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati yaliyotiwa saini kati ya nchi hizo mbili mwishoni mwa mwaka jana.
-
Chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa: Chombo cha Mauaji
Apr 28, 2025 23:16Mauaji ya kudungwa kisu Muislamu nchini Ufaransa ndani ya Msikiti Khadija katika kijiji kilichoko kusini mwa nchi hiyo yameibua maswali mengi kuhusu kuongezeka mivutano ya kijamii na ubaguzi dhidi ya Waislamu, hasa ikitiliwa maanani kwamba chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu (Islamophobia) ni jambo linaloisumbua nchi ya Ufaransa
-
Human Rights Watch yatoa wito wa kushughulikiwa hatari za roboti wauaji
Apr 28, 2025 23:13Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetahadharisha kuhusu hatari kubwa ya silaha zinazojiendesha zenyewe kwa haki za binadamu wakati wa vita na amani.
-
Waziri Mkuu mpya wa Greenland amwambia Trump: Greenland haiuzwi
Apr 28, 2025 23:13Waziri Mkuu mpya wa Greenland amesisitiza kuwa Greenland haiuzwi. Jens Frederik Nielsen ameeleza haya akimhutubu Rais wa Marekani ambaye ametaka eneo hilo kuunganishwa na Marekani.
-
Trump, Rais wa Marekani anayechukiwa zaidi katika miaka 70 iliyopita
Apr 28, 2025 22:46Donald Trump, rais wa Marekani, alirejea kwa mara ya pili Ikulu ya White House akiwa na kiwango cha juu zaidi cha umaarufu tangu kuanza safari yake ya kisiasa. Hata hivyo, utafiti mpya wa mtandao wa habari wa Marekani, CNN, unaonyesha kuwa umaarufu wa Trump umeshuka hadi kiwango cha chini kabisa karibu na siku ya 100 ya kurejea kwake madarakani.
-
Ripoti: Gharama za kijeshi duniani zimeongezeka sana
Apr 28, 2025 07:52Matumizi ya kijeshi ulimwenguni yameongezeka kwa kiwango kikubwa zaidi tangu kumalizika kwa Vita Baridi na kufikia dola trilioni 2.7.