-
Aliyehusika na matukio kadhaa ya kuvunjia heshima Qur'ani aangamizwa
Jan 30, 2025 08:46Salwan Momika mtu aliyezua maandamano na ghasia baada ya kuchoma moto Qur'ani Tukufu ameuawa kwa kupigwa risasi nchini Sweden.
-
Safari za Wazayuni kwenda New Zealand chini ya darubini kali
Jan 29, 2025 22:26Wazayuni wanaofanya safari nchini New Zealand wapo chini ya uangalizii na darubini kali na kufanya mazingira kuwa magumu kwa wale ambao wana historia kuhudumu katika jeshi la Kizayuni.
-
Kwa nini dunia inaendelea kupinga mpango wa kuwalazimisha wakazi wa Gaza kuhama nchi yao?
Jan 29, 2025 22:23Upinzani dhidi ya mpango wa Donald Trump wa kuwalazimisha Wapalestina wa Ukanda wa Gaza kuhama eneo hilo unaendelea. Umoja wa Mataifa pia umepinga suala hilo.
-
Maelfu waandamana Washington kupinga sera za uhamiaji za Trump
Jan 29, 2025 07:20Maelfu ya watu huko Marekani wamefanya maandamano nje ya Ikulu ya White House mjini Washington DC, kupinga mpango wa Rais wa nchi hiyo, Donald Trump wa kusimamisha ufadhili wa serikali, pamoja na sera zake tata za uhamiaji.
-
Waziri Mkuu wa Italia achunguzwa kwa kumuachia huru mshukiwa wa ICC
Jan 29, 2025 07:00Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni amewekwa chini ya uchunguzi wa mahakama kufuatia uamuzi wa serikali yake wa kumwachilia huru afisa wa polisi wa Libya anayesakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC.
-
Umoja wa Ulaya dhidi ya Marekani; Kaja Kallas asisitiza kushikama nchi za Ulaya
Jan 28, 2025 23:57Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa kuna ulazima wa kushikamana nchi za Ulaya mkabala wa Marekani.
-
Huduma mpya za Trump kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Jan 28, 2025 23:05Katika siku za mwanzo za muhula wake wa pili wa uongozi, Donald Trump, rais mpya wa Marekani, kwa mara nyingine tena amefuata njia ile ile aliyopitia katika muhula wa kwanza wa uongozi wake. Katika muhula wa kwanza, Trump alitoa uungaji mkono mkubwa na ambao haujashuhudiwa kwa utawala wa Kizayuni na kuchukua hatua mpya sambamba na kuiunga mkono Israel na kuwapinga Wapalestina. Vitendo na misimamo hii imekutana na majibu chanya kutoka Tel Aviv.
-
EuroMed Rights: Mpango wa Trump ni kuunga mkono mauaji ya Kimbari dhidi ya watu wa Palestina
Jan 28, 2025 05:49Kundi la kutetea haki za binadamu Ulaya-Mashariki ya Kati limeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya pendekezo la hivi karibuni la Donald Trump la kuwahamishia wakazi wa Gaza na kuwapeleka Misri na Jordan, likitoa wito wa kuwepo upinzani mkali wa kikanda na kimataifa dhidi ya wazo hilo.
-
Unajua ni asilimia ngapi ya Waislamu barani Ulaya ambao ni wahanga wa ubaguzi wa rangi?
Jan 28, 2025 05:46Shirika la Umoja wa Ulaya la Haki za Msingi limetangaza kwamba mmoja kati ya kila Waislamu wawili katika Umoja wa Ulaya ni mwathiriwa wa "ubaguzi na ubaguzi wa rangi katika maisha yake ya kila siku."
-
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa: Wanaharakati wakosoaji wa Israel sio wahalifu
Jan 28, 2025 04:31Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na wanaharakati wa mitandao ya kijamii wamelaani vikali kukamatwa kwa mwandishi maarufu wa habari Mmarekani mwenye asili ya Palestina katika mji wa Zurich Uswisi, wakisema kuwa kunazua wasiwasi kuhusu uhuru wa kujieleza katika nchi za Magharibi.