-
Mkuu wa haki za binadamu wa UN awakosoa wanasiasa kwa kukandamiza haki za binadamu
Sep 10, 2024 03:47Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa jana alifungua kikao cha 57 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoisibu dunia ikiwemo machafuko ya kisiasa, kukandamizwa haki za wanawake na uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza.
-
Msemaji wa Umoja wa Mataifa: Hakuna shule zilizobakia Ukanda wa Gaza
Sep 10, 2024 03:02Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa ikiwa ni mwanzo wa mwaka wa masomo katika Ukanda wa Gaza, zaidi ya vijana 600,000 wamenyimwa fursa ya kupata elimu rasmi kwa mwaka mwingine, na kuwa hakuna shule zinazopatikana katika ukanda huo.
-
Erdogan atoa mwito wa kuanzishwa 'Muungano wa Kiislamu' wa kukabiliana na Israel
Sep 09, 2024 03:19Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametoa wito wa kuundwa muungano mpana wa nchi za Kiislamu ili kukabiliana na alichokiita "tishio la kujitanua" linaloonekana kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Wizi wa simu za rununu waongezeka kwa 150% nchini Uingereza
Sep 08, 2024 23:25Uingereza imeshuhudia ongezeko kubwa la viwango vya uhalifu, jambo ambalo sasa linashughulisha sana maoni ya umma. Ongezeko kubwa la visa vya wizi wa mifuko na simu za kisasa za rununu limeifanya serikali ya Uingereza iahidi kuchukua hatua kali dhidi ya uhalifu wa mitaani.
-
Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yafanyika Berlin Ujerumani
Sep 08, 2024 23:24Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina hususan wa Ukanda wa Gaza.
-
UN: Moshi wakati wa kupika uliua watu milioni 3.1 mwaka 2021
Sep 08, 2024 00:57Moshi wakati wa kupika majumbani ulisababisha vifo vya mapema vya watu milioni 3.1 mnamo 2021 ambapo idadi kubwa ya waliofariki ni kutoka bara la Afrika.
-
Ripoti ya GRFC: Sudan na Gaza ni miongoni mwa maeneo yaliyo katika hatari kubwa ya njaa
Sep 07, 2024 23:38Ripoti iliyotolewa na Shirika la Global Report on Food Crises (GRFC) imeeleza kuwa Nigeria, Sudan, Ethiopia, Zimbabwe, Malawi , Chad na eneo la Ukanda wa Gaza ni maeneo ambayo yapo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na njaa huku Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Lebanon mwaka huu zikipata nafuu ya kiwango fulani ikilinganishwa na mwaka jana wa 2023.
-
Baada ya jela zake kujaa, Uingereza inafikiria kuwahamishia wafungwa wake Estonia
Sep 07, 2024 07:29Gazeti la Telegraph limeripoti kuwa, Serikali ya Uingereza inafikiria kukodi nafasi katika magereza ya Estonia kutokana na jela zake kufurika wafungwa.
-
Norway yakata ushirikiano na mashirika yanayoiunga mkono Israel
Sep 05, 2024 23:33Mfuko wa Taifa wa Utajiri wa Norway umetangaza kuwa unakata ushirikiano uliokuwepo baina yake na makampuni yanayouunga mkono utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Mwanamke wa Kimarekani aliyejaribu kumzamisha mtoto wa Kipalestina afunguliwa mashtaka ya jaribio la kuua
Sep 04, 2024 23:01Baraza Kuu la Mahakama ya Tarrant limemfungulia mashtaka mwanamke wa Texas kwa tuhuma za kujaribu kumzamisha msichana mwenye umri wa miaka 3 wa Kipalestina raia wa Marekani, kutokana na chuki za ubaguzi.