-
Mkuu wa mtandao wa fedha wa shirika la ujasusi la Israel Mossad atiwa mbaroni nchini Uturuki
Sep 03, 2024 23:08Polisi wa Istanbul wamemtia mbaroni Liridon Rexhepi, ambaye Shirika la Taifa la Intelijensia la Uturuki (MIT) limemtambua kama Mkuu wa Mtandao wa Fedha wa shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel Mossad ndani ya nchi hiyo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa jana Jumanne na duru za usalama za Uturuki.
-
Afisa wa zamani wa UN: Marekani ni mshirika katika mauaji ya kimbari ya Israel
Sep 03, 2024 09:11Afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa, ambaye alijiuzulu mwaka jana akipinga vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelea kufanywa na utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza ukisaidiwa na Marekani na washirika wake, ameendelea kulaani ushiriki wa Washington katika uhalifu huo.
-
Richard Nephew, mbunifu wa vikwazo dhidi ya Iran akiri kutokuwa na athari wenzo wa vikwazo
Sep 03, 2024 08:19Richard Nephew, mbunifu wa vikwazo dhidi ya Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje na ya Fedha ya Marekani amekiri kutokuwa na taathira na kushindwa kwa mifumo ya vikwazo dhidi ya nchi nyingine.
-
Wananchi wa Marekani waandamana kuwatetea raia wanaodhulumika wa Palestina
Sep 03, 2024 08:10Maelfu ya wakazi wa mji wa New York nchini Marekani wamefanya maandamano kulaani jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
Venezuela yailaani Washington kwa kuiiba ndege yake, yaapa kulipiza kisasi
Sep 03, 2024 03:17Serikali ya Venezuela jana Jumatatu iliilaani vikali Washington kwa kitendo chake cha kuiteka ndege ya Rais Nicolas Maduro wa Venezuela na kukitaja kitendo hicho kuwa ni muendelezo wa uharamia na uhalifu wa Marekani.
-
WHO yasema watoto wa Gaza wanahitaji amani zaidi kuliko chanjo
Sep 03, 2024 01:23Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa (WHO) limesisitiza kuwa "amani" ndilo suluhisho bora zaidi la kuwaokoa watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, wakati kampeni ya chanjo ya polio ikiendelea katika eneo hilo ambalo linakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mgogoro wa kisiasa nchini Ufaransa na hali ngumu inayomkabili Macron
Sep 02, 2024 22:52Mamia ya watu wa Ufaransa wameandamana katika mitaa ya Paris na kukusanyika katika uwanja wa Danfer-Rochereau, wakipiga nara dhidi ya Rais Emmanuel Macron na kumtaka ajiuzulu mora moja.
-
The Guardian: Netanyahu na Trump ni miongoni mwa "waovu wakuu wa karne ya 21"
Sep 02, 2024 03:48Gazeti la The Guardian la Uingereza limeandika kuwa, Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Russia Vladimir Putin, ndio nakala ya mpya ya "watatu waovu" zaidi waliotawala karne iliyopita, na kwamba ni warithi wa Joseph Stalin, Adolf Hitler na Mao Zedong.
-
Waandamanaji Ireland wataka kutimuliwa balozi wa Israel
Sep 01, 2024 23:28Waandamanaji nchini Ireland wameandamana na kukusanyika mbele ya Bunge la nchi hiyo mjini Dublin wakitaka balozi wa utawala wa Kizayuni afukuzwe nchini humo.
-
Guterres: Zichukuliwe hatua kimataifa kumaliza ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika
Sep 01, 2024 06:43Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kimataifa ili “kutokomeza ubaguzi na ubaguzi wa rangi” dhidi ya watu wenye asili ya Afrika.