Wananchi wa Marekani waandamana kuwatetea raia wanaodhulumika wa Palestina
(last modified 2024-09-03T11:40:44+00:00 )
Sep 03, 2024 11:40 UTC
  • Wananchi wa Marekani waandamana kuwatetea raia wanaodhulumika wa Palestina

Maelfu ya wakazi wa mji wa New York nchini Marekani wamefanya maandamano kulaani jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Watu katika maeneo mbalimbali ya dunia na pia huko Marekani wamekuwa wakiandamana katika miezi ya karibuni kuonyesha mshikamano na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na kupinga jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.  

Shirika la habari la Mehr limeripoti kuwa, wananchi nchini Marekani wameandamana katika mji wa New York dhidi ya serikali ya Kizayuni ya Israel na kulaani jinai za mauaji ya kimbari ya utawala huo huko Gaza. 

Waandamanaji wametaka kusimamishwa vita na mauaji ya kimbari ya utawala bandia wa Israell dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.  

Wizara ya Afya ya Palestina katika ukanda huo imetangaza kuwa Wapalestina zadi ya elfu 40 wameuliwa shahidi na zaidi ya elfu 94 kujeruhiwa  tangu Israel ianzishe mashambulizi na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza Oktoba 7 mwaka jana. Asilimia 33 ya mashahidi hawa tajwa ni watoto, asilimia 8.6 wazee na asilimia 18.4 ni wanawake.  

Mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza 

  

Tags