-
Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Uingereza ajiuzulu akipinga uuzaji silaha wa nchi hiyo kwa Israel
Aug 17, 2024 22:55Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Uingereza amejiuzulu wadhifa wake katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo akipinga uuzaji silaha wa nchi hiyo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Mwanadiplomasia huyo amelaani hatua ya serikali ya London ya kuendelea kuiuzia Israel silaha na kuitaja kuwa haiwezi kuhalalishwa.
-
Wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani kuanza tena maandamano ya kupinga mauaji ya kimbari Gaza
Aug 17, 2024 10:07Huku likizo ya majira ya joto ikikaribia kumalizika na kufunguliwa tena vyuo vikuu nchini Marekani, kunashuhudiwa mkakati wa kuanzishwa tena maandamano ya wanafunzi dhidi ya uhalifu na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel ikishirikiana na Marekani huko Gaza.
-
China: Marekani ndio tishio kubwa zaidi la nyuklia duniani
Aug 17, 2024 06:57Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China amesema, Marekani ndiyo hatari kubwa zaidi kwa dunia endapo yatatokea mapigano ya nyuklia.
-
UK iliwapa mafunzo askari wa Ukraine kabla ya kushambulia eneo la Kursk la Russia
Aug 17, 2024 05:54Gazeti la Times linalochapishwa Uingereza limefichua kuwa wanajeshi wa Ukraine walioshiriki katika uvamizi wa vikosi vya Kiev katika mkoa wa Kursk wa Russia, walipewa mafunzo na wataalamu wa kijeshi wa Uingereza katika kipindi cha wiki chache kabla ya kufanyika shambulio hilo la kushtukiza.
-
Umoja wa Ulaya wazitaka nchi wanachama kujiandaa na wimbi la MPOX
Aug 17, 2024 03:40Shirika la afya la Umoja wa Ulaya limezitaka nchi wanachama wa umoja huo kujiandaa na uwezekano wa wagonjwa zaidi wa virusi vya homa ya MPOX.
-
Uholanzi yalaani ukatili wa Wazayuni dhidi ya Wapalestina
Aug 17, 2024 03:39Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uholanzi amelaani mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kutaka ulinzi wa raia.
-
Russia yaonya juu ya hatari ya kuanza Vita vya Tatu vya Dunia
Aug 17, 2024 00:55Mbunge mmoja wa Russia amesema kuwa, wimbi jipya la mashambulizi lililoanzishwa na wanajeshi wa Ukraine ndani ya ardhi ya Russia wakiungwa mkono na nchi za Magharibi hasa Marekani, linaisukuma dunia kwenye shimo la vita vya tatu vikubwa vya dunia nzima.
-
Utafiti: Zaidi ya 50% jamii ya wanadamu hawana maji safi ya kunywa
Aug 17, 2024 00:53Utafiti mpya umefichua kuwa, takriban watu bilioni 4.4 duniani kote hawana maji safi na salama ya kunywa.
-
Athari za jinai za Marekani nchini Afghanistan
Aug 17, 2024 00:52Kundi la Taliban linaloongoza Afghanistan limetoa taarifa likitaja maadhimisho ya kumbukumbu ya kuondoka Marekani nchini humo kuwa ni muhimu, fakhari na Siku ya ushindi kwa nchi hiyo.
-
Mchango wa madola ya Magharibi katika machafuko ya Asia Magharibi
Aug 16, 2024 07:05Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Massoud Pezeshkian amesema kuwa, himaya na uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni ndio sababu kuu na muhimu katika kuhatarisha usalama wa eneo la Magharibi mwa Asia.