-
Umoja wa Mabunge ya OIC walaani kufungwa vituo vya Kiislamu nchini Ujerumani
Aug 16, 2024 07:01Sekretarieti ya Umoja wa Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani kufungwa vituo vya Kiislamu nchini Ujerumani.
-
WHO yaonya kuhusu kuzuka upya kwa kipindupindu katika nchi nyingi duniani
Aug 16, 2024 04:16Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu kuzuka upya ugonjwa wa kipindupindu katika nchi nyingi dunia likisisitiza kuwa jumla ya wagonjwa 307,433 wa kipindupindu na vifo 2,326 vimeripotiwa kutoka nchi 26 kati ya Januari na Julai mwaka huu.
-
Mpox yafika Ulaya baada ya kuua mamia barani Afrika
Aug 16, 2024 00:50Baada ya kuua mamia ya watu barani Afrika, sasa umonjwa wa Mpox umeripotiwa kuingia barani Ulaya hususan Sweden.
-
Marekani: Tunatamani Iran isiishambulie kijeshi Israel
Aug 16, 2024 00:47Mratibu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Ikulu ya Marekani, White House amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bado ina nia ya kujibu mashambulizi na kuutia adabu utawala wa Kizayuni kwa kuupiga kwa silaha lakini amesema kuwa, anatamani Iran isifanye hivyo.
-
Guterres akosoa muundo wa Baraza la Usalama na kuunga mkono uanachama wa mwakilishi wa Afrika katika baraza la UN
Aug 15, 2024 22:57Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametangaza uungaji mkono wake wa kufanyika mabadiliko katika muundo wa Baraza la Usalama na umoja huo na uanachama wa kudumu wa mjumbe wa Afrika katika chombo hicho.
-
Sadiq Khan: Usalama umeimarishwa katika misikiti ya London
Aug 15, 2024 10:45Meya wa jiji la London ametangaza kuongezwa hatua za usalama katika mji huo ikiwa ni pamoja na mafunzo katika misikiti katika mji mkuu huo wa Uingereza.
-
Erdogan: Muundo wa Baraza la Usalama ufanyiwe mabadiliko ya kimsingi
Aug 15, 2024 09:51Rais Recep Tayyib Erdogan wa Uturuki amesema kuwa, muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambao uko mbali na utekelezaji majukumu yake ya kuhakikisha amani na usalama vinatawala duniani, lazima ufanyiwe mabadiliko ya kimsingi.
-
Wanachuo wanaoitetea Palestina 'wakaribisha' kujiuzulu Rais wa Chuo Kikuu cha Columbia
Aug 15, 2024 04:25Rais wa Chuo Kikuu cha Columbia Minouche Shafik alitangaza kujiuzulu jana Jumatano, takriban miezi minne baada ya chuo hicho kushuhudia maandamano ya wananchuo waliokuwa wakilalamikia vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Israel huko Gaza.
-
WHO: Wanaoambukizwa zaidi Mpox ni wanaume kupitia ngono
Aug 15, 2024 04:14Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti kuwa, kesi 9 kati ya 10 za homa ya nyani (Mpox) zinawakabili wanaume, ambapo aghalabu yao wanaambukizwa kwa njia ya zinaa.
-
Japan yasema itaitambua Palestina kwa 'njia kamilifu'
Aug 14, 2024 23:15Serikali ya Japan imesisitiza kwa mara nyingine tena kuwa, inatathmini suala la kulitambua rasmi taifa huru la Palestina.