WHO yaonya kuhusu kuzuka upya kwa kipindupindu katika nchi nyingi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115284-who_yaonya_kuhusu_kuzuka_upya_kwa_kipindupindu_katika_nchi_nyingi_duniani
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu kuzuka upya ugonjwa wa kipindupindu katika nchi nyingi dunia likisisitiza kuwa jumla ya wagonjwa 307,433 wa kipindupindu na vifo 2,326 vimeripotiwa kutoka nchi 26 kati ya Januari na Julai mwaka huu.
(last modified 2024-08-16T04:16:52+00:00 )
Aug 16, 2024 04:16 UTC
  • WHO yaonya kuhusu kuzuka upya kwa kipindupindu katika nchi nyingi duniani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuhusu kuzuka upya ugonjwa wa kipindupindu katika nchi nyingi dunia likisisitiza kuwa jumla ya wagonjwa 307,433 wa kipindupindu na vifo 2,326 vimeripotiwa kutoka nchi 26 kati ya Januari na Julai mwaka huu.

Taarifa ya WHO imesema, Kanda ya Mashariki ya Mediterania ilirekodi idadi kubwa zaidi, ikifuatiwa na Kanda ya Afrika, Kanda ya Kusini-Mashariki mwa Asia, Kanda ya Amerika, na Kanda ya Ulaya.

Mwitikio wa kupambana na kipindupindu unakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na uhaba mkubwa wa chanjo ya ugonjwa huo kwa njia ya kinywa (OCV), huku mahitaji yakizidi ugavi. Tangu Januari 2023, nchi 18 zimeomba dozi milioni 105, karibu mara mbili ya dozi milioni 55 zinazozalishwa katika kipindi hiki.

WHO: Kuna uhaba wa chanjo ya kipindupindu

Mnamo Januari 2023, Shirika la Afya Duniani liliainisha kuibuka tena kwa kipindupindu duniani kama dharura ya daraja la 3, kiwango chake cha juu zaidi cha dharura.

Kwa kuzingatia ongezeko la idadi ya milipuko, kuenea kwake kijiografia na kuendelea uhaba wa chanjo na rasilimali, WHO inaendelea kutaja hatari ya kimataifa maambukizi ya kipindupindu kuwa kubwa sana, na kudumisha hali ya dharura ya daraja la 3.

Shirika la Afya Duniani linasema, ongezeko la joto linaloruhusu bakteria wa kipindupindu kuishi muda mrefu, limezidisha milipuko ya ugonjwa huo na kusababisha viwango vya juu vya vifo katika muongo mmoja wa karibuni.