-
Kitanzi kinazidi kubana koo ya Biden.. Wafadhili waungana na wanasiasa kutaka asigombee urais
Jul 13, 2024 06:00Gazeti la New York Times limeripoti kwamba kundi la wafadhili mashuhuri wa chama cha Democratic wameungana na wanasiasa kupinga jaribio la Joe Biden la kutaka kugombea urais wa Marekani kwa muhula wa pili katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba ijayo.
-
Msimamo wa Erdoğan kuhusu ushirikiano wa NATO na utawala wa Kizayuni
Jul 13, 2024 02:15Rais wa Uturuki amesema kuwa, ushirikiano wa Shirika la la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) na utawala wa Kizayuni wa Israel hauwezi kuendelea kwa sababu utawala huo ghasibu unakiuka thamani na maadili ya kimsingi ya muungano huo.
-
China yatupilia mbali madai ya NATO kwamba, inaisaidia Russia katika vita vya Ukraine
Jul 12, 2024 22:42Serikali ya China imekanusha na kupuuza madai yaliyotolewa na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kwamba, Beijing inaisadia kisilaha Russia katika vita vyake na Ukrane.
-
Uhispania: NATO inapaswa kuacha undumakuwili kuhusu Ukraine na Gaza
Jul 12, 2024 07:58Waziri Mkuu wa Uhispania ametoa wito kwa wanachama wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuheshimu sheria za kimataifa kwa kiwango sawa kuhusiana na Gaza na Ukraine bila "kutumia misimamo na sera za kindumakuwili".
-
Putin: Huenda BRICS ikaunda Bunge lake katika siku zijazo
Jul 11, 2024 23:34Rais Vladimir Putin amedokeza kuwa, yumkini kundi la BRICS la mataifa yanayoinukia kiuchumi duniani likaunda Bunge lake katika mustakabali wa karibu.
-
Netanyahu kutopitia Ulaya akienda US, anahofia kukamatwa
Jul 10, 2024 23:03Waziri Mkuu wa utawala wa Israel, Benjamin Netanyahu amefuta mpango wa kushukia katika moja ya nchi za Ulaya kabla ya kuendelea na safari yake ya kwenda Marekani, akihofia kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) inajiandaa kutoa waranti wa kumtia nguvuni kwa tuhuma za kuhusika na jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza.
-
Rashida Tlaib ataka kukamatwa wahusika wa mauaji ya kimbari huko Khan Yunis
Jul 10, 2024 08:53Mwakilishi wa chama cha Democratic nchini Marekani ameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iamuru kutiwa nguvuni wahusika wa mauaji ya kimbari huko Khan Yunis.
-
Trump amwalika tena Biden kufanya mdahalo mwingine wiki hii
Jul 10, 2024 03:23Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amemwalika mpinzani wake katika uchaguzi, Rais aliyeko madarakani Joe Biden, kufanya mdahalo mwingine wiki hii kama fursa ya "kujiokoa" baada ya utendaji mbaya wa hivi majuzi aliounyesha katika mdahalo huo.
-
Rais wa Bolivia: Mapambano ya Wapalestina ni ya kupigania kurejesha ardhi yao
Jul 09, 2024 22:56Rais wa Bolivia amesema kuwa, mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni kutaka kurejesha ardhi zao zilizoporwa ni haki ya taifa la Palestina.
-
Umoja wa Ulaya uko tayari kuimarisha ushirikiano na Iran
Jul 09, 2024 22:55Msemaji wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema umoja huo uko tayari kwa ajili ya kupanua wigo wa ushirikiano wa pande mbili na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.