-
Takriban 40% ya wanafunzi wa vyuo vikuu Uingereza wanasema shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel ni mapambano ya ukombozi
May 19, 2024 22:46Kura ya maoni iliyochapishwa na gazeti la Uingereza la Daily Mail inaonesha kuwa, karibu 40% ya wanafunzi katika vyuo vikuu vya Russell Group wanaamini kwamba shambulio la Oktoba 7 (operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa) ilikuwa kitendo cha Muqawama na mapambano ya ukombozi ya Wapalestina.
-
Hatua mpya ya Baraza la Wawakilishi la Marekani katika kuunga mkono utawala wa Kizayuni
May 19, 2024 07:55Alhamisi Mei 16, Baraza la Wawakilishi la Marekani, Congress, lilikosoa uamuzi wa hivi karibuni wa Rais Joe Biden wa Marekani wa kuzuia kutumwa shehena ya silaha kwa Israel, na kupasisha mswada chini ya anwani "Misaada kwa ajili ya Usalama wa Israel", ambao ulimtaka Biden asizuie tena kutumwa silaha Israeli kwa kisingizio chochote kile.
-
Polisi wa Marekani wawapiga na kuwatia nguvuni watetezi wa Palestina walioadhimisha Siku ya Nakba
May 19, 2024 07:45Askari polisi wa Marekani wamewapiga na kuwakamata watu kadhaa katika maandamano ya kuiunga mkono Palestina yaliyofanyika katika mji wa Brooklyn jimboni New York, ukiwa ni mwendelezo wa operesheni za kukandamiza na kuzima sauti zinazopinga vita dhidi ya Ghaza nchini Marekani.
-
Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko nchini Afghanistan yafikia watu 400
May 19, 2024 07:12Idadi ya vifo vilivyosababishwa na mvua kubwa na mafuriko yaliyoikumba Afghanistan imefikia 400 baada ya watu wengine 18 kufariki dunia kutokana na mafuriko hayo.
-
Russia: Umoja wa Ulaya hauna uvumilivu katika suala la uhuru wa kutoa maoni
May 19, 2024 07:09Spika wa Bunge la Russia Duma ameushutumu Umoja wa Ulaya (EU) kwa kubana maoni mbadala na kuminya uhuru wa kujieleza kwa lengo la kuwahadaa raia.
-
Maandamano ya 14 makubwa tangu Oktoba ya kuunga mkono Palestina yafanyika London
May 18, 2024 23:17Maandamano ya 14 makubwa kuwahi kushuhudiwa tangu mwezi Oktoba 2023 katika mji mkuu wa Uingereza, London ya kuunga mkono Palestina, yalifanyika jana Jumamosi katika ukumbi wa White Hall, kwenye kitovu cha majengo ya serikali na karibu mno na Downing Street, yalipo makazi na ofisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo.
-
Washington Post: Wafanyabiashara wa Marekani wamechochea ukandamizaji wa polisi dhidi ya harakati za kutetea Palestina kwenye vyuo vikuu
May 18, 2024 09:11Gazeti la Washington Post lilmefichua kuwa kundi la mabilionea wa Kimarekani, akiwemo mwanzilishi wa Starbucks, wamemshinikiza Meya wa New York kutuma polisi ili kuvunja maandamano ya watetezi wa Palestina katika Chuo Kikuu cha Columbia.
-
Russia: Magharibi inacheza na moto
May 18, 2024 09:11Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametangaza kwamba nchi za Magharibi zinataka kuzidisha mvutano na zinacheza na moto kwa kuipatia silaha na kuihimiza Ukraine kushambulia ardhi ya Russia.
-
FAO: Hatua za kupunguza athari za El Nino kwa usalama wa chakula zimezaa matunda
May 18, 2024 09:08Hatua zilizochukuliwa miaka miwili iliyopita na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ili kupunguza athari mbaya za mvua za El Niño katika nchi 23 duniani zimelinda usalama wa chakula na maisha ya watu zaidi ya milioni 1.6.
-
Muhammad ni jina la pili maarufu nchini Uingereza
May 18, 2024 04:16Jina la Mtume Mtukufu (S.A.W) ni jina la pili wanalopewa watoto wachanga nchini Uingereza huku Waislamu wakiunda asilimia sita na nusu tu ya jamii ya nchi hiyo.